SEARCH DATABASE
The Global Gender Equality Constitutional Database is a repository of gender equality related provisions in 194 constitutions from around the world. The Database was updated in partnership with the International Bar Association's Human Rights Institute (IBAHRI) and with support from the Swedish International Development Agency (SIDA) and the Government of Japan. Experience its wealth and depth of information by starting your search now.
ABOUT 13 RESULTS
Judicial Protection
Kenya
- English(1) The High Court has jurisdiction, in accordance with Article 165, to hear and determine applications for redress of a denial, violation or infringement of, or threat to, a right or fundamental freedom in the Bill of Rights.
(2) Parliament shall enact legislation to give original jurisdiction in appropriate cases to subordinate courts to hear and determine applications for redress of a denial, violation or infringement of, or threat to, a right or fundamental freedom in the Bill of Rights.
(3) In any proceedings brought under Article 22, a court may grant appropriate relief, including—
(a) a declaration of rights;
(b) an injunction;
(c) a conservatory order;
(d) a declaration of invalidity of any law that denies, violates, infringes, or threatens a right or fundamental freedom in the Bill of Rights and is not justified under Article 24;
(e) an order for compensation; and
(f) an order of judicial review. (Art. 23) - Swahili(1) Mahakama Kuu ina mamlaka, kwa mujibu wa Kifungu cha 165, ya kusikia na kuamua maombi ya kutoa fidia ya kukataliwa, kukiuka au kuvunja, au kutishia, haki au uhuru wa msingi katika Sheria ya Haki za Binadamu.
(2) Bunge litatunga sheria ili kutoa mamlaka ya asili katika kesi stahiki ili kuiamuru mahakama kusikiliza na kuamua maombi ya kutoa fidia ya kukataliwa, kukiuka au kuvunja, au kutishia, haki au uhuru wa msingi katika Sheria ya Haki za Binadamu.
(3) Katika kesi yoyote iliyofunguliwa chini ya Kifungu cha 22, mahakama inaweza kutoa unafuu stahiki, ikiwa ni pamoja na—
(a) kutangaza haki;
(b) kutoa amri ya kisheria;
(c) amri ya kuhifadhi;
(d) tamko la kuharamisha sheria yoyote ambayo inanyima, inakiuka, inavunja, au inatishia haki au uhuru wa msingi katika Sheria ya Haki za Binadamu na haijathibitishwa chini ya kifungu cha 24;
(e) amri ya kutoa fidia; na
(f) amri ya kufanya mapitio ya sheria. (Kifungu cha 23)
National Human Rights Bodies
Kenya
- English…
(11) The chairperson and vice-chairperson of a commission6 shall not be of the same gender.
… (Art. 250) - Swahili…
(11) Mwenyeketi na makamu mwenyekiti wa tume hawatakuwa wa jinsia moja.
… (Kifungu cha 250)
National Human Rights Bodies
Kenya
- English(1) There is established the Kenya National Human Rights and Equality Commission.
(2) The functions of the Commission are—
(a) to promote respect for human rights and develop a culture of human rights in the Republic;
(b) to promote gender equality and equity generally and to coordinate and facilitate gender mainstreaming in national development;
(c) to promote the protection, and observance of human rights in public and private institutions;
(d) to monitor, investigate and report on the observance of human rights in all spheres of life in the Republic, including observance by the national security organs;
(e) to receive and investigate complaints about alleged abuses of human rights and take steps to secure appropriate redress where human rights have been violated;
(f) on its own initiative or on the basis of complaints, to investigate or research a matter in respect of human rights, and make recommendations to improve the functioning of State organs;
(g) to act as the principal organ of the State in ensuring compliance with obligations under treaties and conventions relating to human rights;
…
(3) Every person has the right to complain to the Commission, alleging that a right or fundamental freedom in the Bill of Rights has been denied, violated or infringed, or is threatened.
(4) Parliament shall enact legislation to give full effect to this Part, and any such legislation may restructure the Commission into two or more separate commissions.
… (Art. 59) - Swahili(1) Kuna Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu na Usawa ya Kenya.
(2) Kazi za Tume ni—
(a) kuimarisha heshima kwa haki za binadamu na kuendeleza utamaduni wa haki za binadamu katika Jamhuri;
(b) kuimarisha usawa wa kijinsia na haki kwa jumla na kuratibu na kuwezesha ujumuishaji wa masuala ya kijinsia katika maendeleo ya kitaifa;
(c) kuimarisha ulinzi, na uzingatiaji wa haki za binadamu katika taasisi za umma na binafsi;
(d) kufuatilia, kuchunguza na kutoa taarifa juu ya uzingatiaji wa haki za binadamu katika nyanja zote za maisha katika Jamhuri, ikiwa ni pamoja na vyombo vya usalama vya kitaifa kuzingatia;
(e) kupokea na kuchunguza malalamiko kuhusu tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu na kuchukua hatua za kutoa fidia stahiki pale ambapo haki za binadamu zimekiukwa;
(f) kwa jitihada zake yenyewe au kwa msingi wa malalamiko, kuchunguza au kutafiti jambo kuhusu haki za binadamu, na kutoa mapendekezo ya kuboresha utendaji kazi wa vyombo vya Serikali;
(g) kufanya kazi kama chombo kikuu cha Serikali katika kuhakikisha uzingatiaji wa majukumu chini ya makubaliano na mikataba inayohusiana na haki za binadamu;
…
(3) Kila mtu ana haki ya kulalamika mbele ya Tume, akidai kuwa haki au uhuru wa msingi katika Sheria ya Haki za Binadamu imenyimwa, imekiukwa au kuvunjwa, au imetishiwa.
(4) Bunge litatunga sheria kuwezesha utekelezaji kamili wa Sehemu hii, na sheria yoyote ya namna hiyo inaweza kuiunda upya tume na kuwa tume tofauti mbili au zaidi.
… (Kifungu cha 59)