SEARCH DATABASE
The Global Gender Equality Constitutional Database is a repository of gender equality related provisions in 194 constitutions from around the world. The Database was updated in partnership with the International Bar Association's Human Rights Institute (IBAHRI) and with support from the Swedish International Development Agency (SIDA) and the Government of Japan. Experience its wealth and depth of information by starting your search now.
ABOUT 143 RESULTS
Affirmative Action (Broadly)
Kenya
- EnglishParliament shall enact legislation to promote the representation in Parliament of—
(a) women;
(b) persons with disabilities;
(c) youth;
(d) ethnic and other minorities; and
(e) marginalised communities. (Art. 100) - SwahiliBunge litatunga sheria ili kuimarisha uwakilishi Bungeni wa—
(a) wanawake;
(b) watu wenye ulemavu;
(c) vijana;
(d) kabila na watu wengine wenye uwakilishi mdogo katika jamii; na
(e) jamii zilizotengwa. (Kifungu cha 100)
Affirmative Action (Broadly)
Kenya
- English(1) Every person is equal before the law and has the right to equal protection and equal benefit of the law.
(2) Equality includes the full and equal enjoyment of all rights and fundamental freedoms.
(3) Women and men have the right to equal treatment, including the right to equal opportunities in political, economic, cultural and social spheres.
(4) The State shall not discriminate directly or indirectly against any person on any ground, including race, sex, pregnancy, marital status, health status, ethnic or social origin, colour, age, disability, religion, conscience, belief, culture, dress, language or birth.
(5) A person shall not discriminate directly or indirectly against another person on any of the grounds specified or contemplated in clause (4).
(6) To give full effect to the realisation of the rights guaranteed under this Article, the State shall take legislative and other measures, including affirmative action3 programmes and policies designed to redress any disadvantage suffered by individuals or groups because of past discrimination.
(7) Any measure taken under clause (6) shall adequately provide for any benefits to be on the basis of genuine need.
(8) In addition to the measures contemplated in clause (6), the State shall take legislative and other measures to implement the principle that not more than two-thirds of the members of elective or appointive bodies shall be of the same gender. (Art. 27) - Swahili(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
(2) Haki sawa ni pamoja na kurufahia kikamilifu na kwa usawa haki zote na uhuru wa msingi.
(3) Wanawake na wanaume wana haki ya kutendewa kwa usawa, ikiwa ni pamoja na haki ya kuwa na fursa sawa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.
(4) Serikali haitambagua mtu yeyote kwa dhahiri au si kwa dhahiri kwa msingi wowote ikiwa ni pamoja na mbari, jinsi, mimba, hali ya ndoa, hali ya afya, asili ya kikabila au kijamii, rangi, umri, ulemavu, dini, dhamiri, imani, utamaduni, mavazi, lugha au kuzaliwa.
(5) Mtu yeyote hatambagua mtu yeyote kwa dhahiri ama si kwa dhahiri kwa misingi yoyote iliyobaisnishwa katika ibara ya (4).
(6) Ili kutekeleza kikamilifu utekelezaji wa haki zilizohakikishwa chini ya Ibara hii, Serikali itachukua hatua za kisheria na hatua nyinginezo, pamoja na mipango na sera thabiti za utekelezaji zilizoundwa ili kufidia unyimwaji wa haki ambao uliwapata watu au kikundi cha watu kwa sababu ya ubaguzi wa zamani.
(7) Hatua yoyote inayochukuliwa chini ya ibara ya (6) itatoa kikamilifu maslahi kwa msingi wa hitaji la kweli.
(8) Pamoja na hatua zilizobainishwa katika ibara ya (6), Serikali itachukua hatua za kisheria na hatua nyinginezo ili kutekeleza kanuni ambayo itahakikisha kwamba washirika wa bodi wa kuchaguliwa au kuteuliwa wa jinsia moja hawatakuwa zaidi ya theluthi mbili. (Kifungu cha 27)
Affirmative Action (Broadly)
Kenya
- English…
(11) The chairperson and vice-chairperson of a commission4 shall not be of the same gender.
… (Art. 250) - Swahili…
(11) Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa tume hawatakuwa wa jinsia moja.
… (Kifungu cha 250)
Affirmative Action (Broadly)
Kenya
- English(1) The Judicial Service Commission shall promote and facilitate the independence and accountability of the judiciary and the efficient, effective and transparent administration of justice …
(2) In the performance of its functions, the Commission shall be guided by the following—
...
(b) the promotion of gender equality. (Art. 172) - Swahili(1) Tume ya Huduma ya Mahakama itakuza na kuwezesha uhuru na uwajibikaji wa mahakama na usimamizi wa haki wenye ufanisi na wenye matokeo yanayotarajiwa na wa uwazi ...
(2) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume itaongozwa na mambo yafuatayo—
...
(b) uimarishaji wa usawa wa kijinsia. (Kifungu cha 172)
Citizenship and Nationality
Kenya
- English(1) A person who has been married to a citizen for a period of at least seven years is entitled on application to be registered as a citizen.
(2) A person who has been lawfully resident in Kenya for a continuous period of at least seven years, and who satisfies the conditions prescribed by an Act of Parliament, may apply to be registered as a citizen.
(3) A child who is not a citizen, but is adopted by a citizen, is entitled on application to be registered as a citizen.
(4) Parliament shall enact legislation establishing conditions on which citizenship may be granted to individuals who are citizens of other countries.
… (Art. 15) - Swahili(1) Mtu ambaye ameolewa na raia kwa muda wa angalau miaka saba ana haki ya kutuma maombi na kuandikishwa kuwa raia.
(2) Mtu ambaye amekaa kihalali nchini Kenya kwa kipindi kisichozidi miaka saba mfululizo, na ambaye anakidhi masharti yaliyowekwa na Sheria ya Bunge, anaweza kutuma maombi ili kuandikishwa kama raia.
(3) Mtoto ambaye si raia, lakini ameasiliwa na raia, ana haki ya kutuma maombi ya kuandikishwa kama raia.
(4) Bunge litatunga sheria ya kuweka masharti ambayo kwayo uraia unaweza kutolewa kwa watu ambao ni raia wa nchi zingine.
… (Kifungu cha 15)
Citizenship and Nationality
Kenya
- English(1) A person is a citizen by birth if on the day of the person’s birth, whether or not the person is born in Kenya, either the mother or father of the person is a citizen.
(2) Clause (1) applies equally to a person born before the effective date, whether or not the person was born in Kenya, if either the mother or father of the person is or was a citizen.
(3) Parliament may enact legislation limiting the effect of clauses (1) and (2) on the descendents of Kenyan citizens who are born outside Kenya.
(4) A child found in Kenya who is, or appears to be, less than eight years of age, and whose nationality and parents are not known, is presumed to be a citizen by birth.
(5) A person who is a Kenyan citizen by birth and who has ceased to be a Kenyan citizen because the person acquired citizenship of another country, is entitled on application to regain Kenyan citizenship. (Art. 14) - Swahili(1) Mtu ni raia kwa kuzaliwa ikiwa siku ya kuzaliwa mtu huyo, iwe mtu huyo amezaliwa Kenya au la, mama au baba wa mtu huyo ni raia.
(2) Ibara ya (1) inatumika sawa kwa mtu aliyezaliwa kabla ya tarehe ya utekelezaji, iwe mtu huyo alizaliwa Kenya au la, ikiwa mama au baba wa mtu huyo ni raia au alikuwa raia.
(3) Bunge linaweza kutunga sheria ili kuweka mipaka ya taathira ya ibara ya (1) na ya (2) kwa vizazi vya raia wa Kenya ambao wamezaliwa nje ya Kenya.
(4) Mtoto aliyepatikana nchini Kenya ambaye, au anaonekana kuwa na umri chini ya miaka minane, na ambaye utaifa na wazazi hawajulikani, anachukuliwa kuwa ni raia kwa kuzaliwa.
(5) Mtu ambaye ni raia wa Kenya kwa kuzaliwa na ameacha kuwa raia wa Kenya kwa sababu mtu huyo alipata uraia wa nchi nyingine, ana haki ya kutuma maombi ya kupata uraia wa Kenya. (Kifungu cha 14)
Citizenship and Nationality
Kenya
- English…
3. ... citizenship.
… (Fourth Schedule - Distribution of Functions between the National Government and the County Governments, Part 1 – National Government) - Swahili…
3. ... uraia.
… (Kiambatisho cha Nne - Mgawanyo wa Majukumu baina ya Serikaili ya Kitaifa na Serikili za Kaunti, Sehemu ya 1 - Serikali ya Kitaifa)
Citizenship and Nationality
Kenya
- English(1) Every person who was a citizen immediately before the effective date retains the same citizenship status as of that date.
(2) Citizenship may be acquired by birth or registration.
(3) Citizenship is not lost through marriage or the dissolution of marriage. (Art. 13) - Swahili(1) Kila mtu ambaye alikuwa raia muda mfupi kabla ya tarehe ya utekelezaji anabaki na hadhi iyo hiyo ya uraia hadi kufikia tarehe hiyo.
(2) Uraia unaweza kupatikana kwa kuzaliwa au kujiandikisha.
(3) Uraia haupotei kwa njia ya ndoa au kuvunjika kwa ndoa. (Kifungu cha 13)
Citizenship and Nationality
Kenya
- EnglishParliament shall enact legislation—
(a) prescribing procedures by which a person may become a citizen;
…
(e) prescribing procedures for revocation of citizenship;
…
(g) generally giving effect to the provisions of this Chapter.
… (Art. 18) - SwahiliBunge litatunga sheria—
(a) ikielezea taratibu ambazo kwazo mtu anaweza kuwa raia;
…
(e) ikielezea taratibu za kufuta uraia;
…
(g) kwa ujumla itakayotekeleza vifungu vya Sura hii.
… (Kifungu cha 18)
Citizenship and Nationality
Kenya
- English...
(2) The citizenship of a person who was presumed to be a citizen by birth, as contemplated in Article 14(4), may be revoked if—
(a) the citizenship was acquired by fraud, false representation or concealment of any material fact by any person;
(b) the nationality or parentage of the person becomes known, and reveals that the person was a citizen of another country; or
(c) the age of the person becomes known, and reveals that the person was older than eight years when found in Kenya. (Art. 17) - Swahili...
(2) Uraia wa mtu ambaye alidhaniwa kuwa raia kwa kuzaliwa, kama ilivyobainishwa katika Kifungu cha 14 (4), unaweza kubatilishwa ikiwa—
(a) uraia huo ulipatikana kwa njia ya udanganyifu, utambulisho wa uongo au kuficha ukweli wowote halisi unaofanywa na yeyote
(b) utaifa au wazazi wa mtu huyo kujulikana, na kuonyesha ukweli kuwa mtu huyo alikuwa raia wa nchi nyingine; au
(c) umri wa mtu huyo kujulikana, na kuonyesha kuwa mtu huyo alikuwa na umri zaidi ya miaka minane alipokutwa Kenya. (Kifungu cha 17)