SEARCH DATABASE
The Global Gender Equality Constitutional Database is a repository of gender equality related provisions in 194 constitutions from around the world. The Database was updated in partnership with the International Bar Association's Human Rights Institute (IBAHRI) and with support from the Swedish International Development Agency (SIDA) and the Government of Japan. Experience its wealth and depth of information by starting your search now.
ABOUT 7 RESULTS
Legislature
Kenya
- English(1) There is established a Parliament of Kenya, which shall consist of the National Assembly and the Senate.
(2) The National Assembly and the Senate shall perform their respective functions in accordance with this Constitution. (Art. 93) - Swahili(1) Kuna Bunge la Kenya, ambalo litaundwa na Bunge la Kitaifa na Seneti.
(2) Vyombo vya Bunge la Kitaifa na Seneti vitafanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba hii. (Kifungu cha 93)
Legislature
Kenya
- EnglishParliament shall enact legislation to promote the representation in Parliament of—
(a) women;
(b) persons with disabilities;
(c) youth;
(d) ethnic and other minorities; and
(e) marginalised communities. (Art. 100) - SwahiliBunge litatunga sheria ili kuimarisha uwakilishi Bungeni wa—
(a) wanawake;
(b) watu wenye ulemavu;
(c) vijana;
(d) kabila na watu wengine wenye uwakilishi mdogo katika jamii; na
(e) jamii zilizotengwa. (Kifungu cha 100)
Legislature
Kenya
- English(1) Elections for the seats in Parliament provided for under Articles 97(1) (c) and 98 (1) (b), (c) and (d), and for the members of county assemblies under 177 (1) (b) and (c), shall be on the basis of proportional representation by use of party lists.
(2) The Independent Electoral and Boundaries Commission shall be responsible for the conduct and supervision of elections for seats provided for under clause (1) and shall ensure that—
…
(b) except in the case of the seats provided for under Article 98 (1) (b), each party list comprises the appropriate number of qualified candidates and alternates between male and female candidates in the priority in which they are listed;
… (Art. 90) - Swahili(1) Uchaguzi wa viti katika Bunge vilivyobainishwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c) na 98 (1) (b), (c) na (d), na kwa wajumbe wa mabunge ya kaunti chini ya kifungu cha 177 (1) (b) na (c), zitakuwa kwa msingi wa uwakilishi wa usawa kwa kutumia orodha za chama.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itakuwa na jukumu la kufanya na kusimamia uchaguzi wa viti vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1) na itahakikisha kwamba—
…
(b) isipokuwa katika viti vilivyobainishwa chini ya Kifungu cha 98 ( 1)(b), orodha ya kila chama inajumuisha idadi inayofaa ya wagombea wenye sifa na wanabadilishana kati ya wagombea wa kiume na wa kike katika kipaumbele ambacho kwacho wameorodheshwa;
… (Kifungu cha 90)
Legislature
Kenya
- English(1) Unless disqualified under clause (2), a person is eligible for election as a member of Parliament if the person—
(a) is registered as a voter;
(b) satisfies any educational, moral and ethical requirements prescribed by this Constitution or by an Act of Parliament; and
(c) is nominated by a political party, or is an independent candidate who is supported—
(i) in the case of election to the National Assembly, by at least one thousand registered voters in the constituency; or
(ii) in the case of election to the Senate, by at least two thousand registered voters in the county.
… (Art. 99) - Swahili(1) Isipokuwa kama hana sifa chini ya ibara ya (2), mtu anastahili kuchaguliwa kama mbunge ikiwa mtu huyo—
(a) ameandikishwa kama mpiga kura;
(b) anakidhi matakwa yoyote ya kielimu, ya kiadili na kimaadili yaliyowekwa na Katiba hii au na Sheria ya Bunge; na
(c) ameteuliwa na chama cha siasa, au ni mgombea huru anayeungwa mkono—
(i) katika suala la uchaguzi wa Bunge la Kitaifa na wapiga kura angalau elfu moja walioandikishwa katika jimbo hilo la uchaguzi; au
(ii) katika suala la uchaguzi wa Seneti, na angalau wapiga kura elfu mbili walioandikishwa katika kaunti husika.
… (Kifungu cha 99)
Legislature
Kenya
- English(1) The Senate consists of—
(a) forty-seven members each elected by the registered voters of the counties, each county constituting a single member constituency;
(b) sixteen women members who shall be nominated by political parties according to their proportion of members of the Senate elected under clause (a) in accordance with Article 90;
(c) two members, being one man and one woman, representing the youth;
(d) two members, being one man and one woman, representing persons with disabilities; and
(e) the Speaker, who shall be an ex officio member.
(2) The members referred to in clause (1) (c) and (d) shall be elected in accordance with Article 90.
(3) Nothing in this Article shall be construed as excluding any person from contesting an election under clause (1) (a). (Art. 98) - Swahili(1) Bunge la Seneti linaundwa na -
(a) wajumbe arobaini na saba kila mmoja aliyechaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa wa kaunti husika, kila kaunti inaunda eneo bunge moja;
(b) wajumbe wanawake kumi na sita ambao watachaguliwa na vyama vya siasa kulingana na idadi yao ya wajumbe wa Seneti waliochaguliwa chini ya ibara ya (a) kwa mujibu wa Kifungu cha 90;
(c) wajumbe wawili, mmoja akiwa mwanaume na mwingine mwanamke wakiwakilisha vijana;
(d) wajumbe wawili, mmoja akiwa mwanaume na mwingine mwanamke wakiwakilisha watu wenye ulemavu; na
(e) Spika, ambaye atakuwa mjumbe kwa nafasi yake.
(2) Wajumbe waliotajwa katika ibara ya (1) (c) na (d) watachaguliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 90.
(3) Hakuna chochote katika Kifungu hiki kitachukuliwa kama kumwondoa mtu yeyote kugombea kwenye uchaguzi chini ya ibara ya (1) (a). (Kifungu cha 98)
Legislature
Kenya
- English(1) The National Assembly consists of—
(a) two hundred and ninety members, each elected by the registered voters of single member constituencies;
(b) forty-seven women, each elected by the registered voters of the counties, each county constituting a single member constituency;
(c) twelve members nominated by parliamentary political parties according to their proportion of members of the National Assembly in accordance with Article 90, to represent special interests including the youth, persons with disabilities and workers; and
(d) the Speaker, who is an ex officio member.
(2) Nothing in this Article shall be construed as excluding any person from contesting an election under clause (1) (a). (Art. 97) - Swahili(1) Bunge la Kitaifa linaundwa na—
(a) wabunge mia mbili na tisini, kila mmoja aliyechaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa kutoka katika eneo bunge moja;
(b) wanawake arobaini na saba, kila mmoja aliyechaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa wa kaunti, kila kaunti inaunda eneo bunge moja;
(c) wajumbe kumi na wawili walioteuliwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni kulingana na idadi yao ya wajumbe wa Bunge la Kitaifa kwa mujibu wa Kifungu cha 90, ili kuwakilisha masilahi maalumu ikiwa ni pamoja na vijana, watu wenye ulemavu na wafanyikazi; na
(d) Spika, ambaye ni mjumbe kwa nafasi yake.
(2) Hakuna chochote katika Kifungu hiki kitachukuliwa kama kumwondoa mtu yeyote kugombea kwenye uchaguzi chini ya ibara ya (1) (a). (Kifungu cha 97)
Legislature
Kenya
- English1. The legislative authority of the Republic is derived from the people and, at the national level, is vested in and exercised by Parliament.
… (Art. 94) - Swahili1. Mamlaka ya kisheria ya Jamhuri yanatoka kwa watu na, kwa kiwango cha kitaifa, yanakabidhiwa na kutekelezwa na Bunge.
… (Kifungu cha 94)