SEARCH DATABASE
The Global Gender Equality Constitutional Database is a repository of gender equality related provisions in 194 constitutions from around the world. The Database was updated in partnership with the International Bar Association's Human Rights Institute (IBAHRI) and with support from the Swedish International Development Agency (SIDA) and the Government of Japan. Experience its wealth and depth of information by starting your search now.
ABOUT 143 RESULTS
Limitations and/or Derogations
Kenya
- English...
(6) Any legislation enacted in consequence of a declaration of a state of emergency—
(a) may limit a right or fundamental freedom in the Bill of Rights only to the extent that—
(i) the limitation is strictly required by the emergency; and
(ii) the legislation is consistent with the Republic’s obligations under international law applicable to a state of emergency; and
(b) shall not take effect until it is published in the Gazette.
… (Art. 58) - Swahili...
(6) Sheria yoyote iliyotungwa kwa sababu ya tangazo la hali ya dharura-
(a) inaweza kuwekea mpaka haki au uhuru wa msingi katika Sheria ya Haki za Binadamu ni kwa kiwango ambacho tu-
(i) mpaka huo unahitajika kabisa na dharura hiyo; na
(ii) sheria hiyo inaoana na majukumu ya Jamhuri chini ya sheria za kimataifa zinazotumika kwa hali ya dharura; na
(b) haitaanza kutekelezwa hadi itakapochapishwa kwenye gazeti la serikali.
… (Kifungu cha 58)
Limitations and/or Derogations
Kenya
- EnglishDespite any other provision in this Constitution, the following rights and fundamental freedoms shall not be limited—
(a) freedom from torture and cruel, inhuman or degrading treatment or punishment;
(b) freedom from slavery or servitude;
(c) the right to a fair trial; and
(d) the right to an order of habeas corpus. (Art. 25) - SwahiliLicha ya sheria nyingineyo yoyote katika Katiba hii, uhuru wa msingi na haki zifuatazo hazitawekewa mipaka-
(a) uhuru dhidi ya kuteswa na ukatili, unyanyasaji au udhalilishaji au adhabu;
(b) uhuru dhidi ya utumwa au kutumikishwa;
(c) haki ya kushtakiwa kwa haki; na
(d) haki ya amri ya kumfikisha mfungwa kortini. (Kifungu cha 25)
Limitations and/or Derogations
Kenya
- English(1) A right or fundamental freedom in the Bill of Rights shall not be limited except by law, and then only to the extent that the limitation is reasonable and justifiable in an open and democratic society based on human dignity, equality and freedom, taking into account all relevant factors including—
(a) the nature of the right or fundamental freedom;
(b) the importance of the purpose of the limitation;
(c) the nature and extent of the limitation;
(d) the need to ensure that the enjoyment of rights and fundamental freedoms by any individual does not prejudice the rights and fundamental freedoms of others; and
(e) the relation between the limitation and its purpose and whether there are less restrictive means to achieve the purpose.
(2) Despite clause (1), a provision in legislation limiting a right or fundamental freedom—
(a) in the case of a provision enacted or amended on or after the effective date, is not valid unless the legislation specifically expresses the intention to limit that right or fundamental freedom, and the nature and extent of the limitation;
(b) shall not be construed as limiting the right or fundamental freedom unless the provision is clear and specific about the right or freedom to be limited and the nature and extent of the limitation; and
(c) shall not limit the right or fundamental freedom so far as to derogate from its core or essential content.
(3) The State or a person seeking to justify a particular limitation shall demonstrate to the court, tribunal or other authority that the requirements of this Article have been satisfied.
(4) The provisions of this Chapter on equality shall be qualified to the extent strictly necessary for the application of Muslim law before the Kadhis’ courts, to persons who profess the Muslim religion, in matters relating to personal status, marriage, divorce and inheritance.
… (Art. 24) - Swahili(1) Haki au uhuru wa msingi katika Sheria ya Haki za Binadamu haitakuwa na mpaka isipokuwa kwa sheria, na tena kwa kiwango ambacho mpaka huo una mantiki na unathibitika kwenye jamii ya uwazi na ya kidemokrasia kwa msingi wa utu wa binadamu, usawa na uhuru, kwa kuzingatia mambo yote muhimu ikiwa ni pamoja na—
(a) asili ya uhuru au haki ya msingi;
(b) umuhimu wa madhumuni ya mpaka huo;
(c) asili na kiwango cha mpaka huo;
(d) hitaji la kuhakikisha kuwa unufaikaji wa uhuru wa msingi na haki kwa mtu yeyote hauathiri uhuru wa msingi na haki ya watu wengine; na
(e) uhusiano kati ya mpaka na madhumuni yake na ikiwa kuna njia zenye ugumu kidogo za kufikia kusudi hilo.
(2) Licha ya ibara ya (1), kifungu katika sheria kinachozuia haki au uhuru wa msingi-
(a) ikiwa kuna sheria iliyotungwa au kufanyiwa marekebisho tarehe hiyo au baada ya tarehe ya utekelezaji, si halali isipokuwa sheria hiyo ielezee kwa umahususi kusudi la kuwekea mipaka haki hiyo au uhuru wa msingi na asili na kiwango cha mpaka huo;
(b) haitachukuliwa kuwa inaiwekea mpaka haki au uhuru wa msingi kama sheria hiyo haiko dhahiri na mahususi kuhusu uhuru wa msingi na haki ambayo itawekewa mipaka na asili na kiwango cha mpaka huo; na
(c) haitawekea mipaka haki au uhuru wa msingi hadi kufikia kiwango cha kupunguza kwenye maudhui yake ya msingi au muhimu.
(3) Serikali au mtu anayetafuta kuhalalisha mpaka fulani ataielezea mahakama, baraza au mamlaka nyingineyo kwamba matakwa ya Kifungu hiki yamekamilishwa.
(4) Sheria za Sura hii juu ya usawa zitahalalishwa kwa kiwango ambacho ni lazima kabisa kutumia sharia ya Kiislamu mbele ya mahakama za Kadhi, kwa watu ambao ni waumini wa dini ya Kiisilamu, katika maswala yanayohusu hadhi ya binafsi, ndoa, talaka na urithi.
… (Kifungu cha 24)
Limitations and/or Derogations
Kenya
- English...
(3) The rights and fundamental freedoms in the Bill of Rights—
(a) belong to each individual and are not granted by the State;
(b) do not exclude other rights and fundamental freedoms not in the Bill of Rights, but recognised or conferred by law, except to the extent that they are inconsistent with this Chapter; and
(c) are subject only to the limitations contemplated in this Constitution. (Art. 19) - Swahili...
(3) Haki na uhuru wa msingi katika Sheria ya Haki za Binadamu-
(a) ni ya kila mtu na haitolewi na Serikali;
(b) haiondoi haki nyinginezo na uhuru wa msingi ambao haupo kwenye Sheria ya Haki za Binadamu, lakini hutambuliwa au hutolewa na sheria, isipokuwa kwa kiwango ambacho zipo kinyume na Sura hii; na
(c) huzingatia tu mipaka iliyobainishwa katika Katiba hii. (Kifungu cha 19)
Marriage and Family Life
Kenya
- English...
(5) The jurisdiction of a Kadhis’ court shall be limited to the determination of questions of Muslim law relating to personal status, marriage, divorce or inheritance in proceedings in which all the parties profess the Muslim religion and submit to the jurisdiction of the Kadhi’s courts. (Art. 170) - Swahili...
(5) Mamlaka ya Mahakama ya Kadhi yatakuwa na mipaka itakayoishia katika kuamua shauri la sheria ya Kiisilamu inayohusiana na hadhi binafsi, ndoa, talaka au urithi katika kesi ambazo kwazo pande zote ni waumini wa dini ya Kiislamu na wanaitii mamlaka ya mahakama za Kadhi. (Kifungu cha 170)
Marriage and Family Life
Kenya
- EnglishWe, the people of Kenya - …
COMMITTED to nurturing and protecting the well-being of the individual, the family, communities and the nation:
… (Preamble) - SwahiliSisi, wananchi wa Kenya -…
TUKIWA TUMEJIZATITI kulea na kulinda maslahi ya mtu, familia, jamii na taifa:
... (Utangulizi)
Marriage and Family Life
Kenya
- EnglishParliament shall—
...
(c) enact legislation—
…
(iii) to regulate the recognition and protection of matrimonial property and in particular the matrimonial home during and on the termination of marriage;
… (Art. 68) - SwahiliBunge-
…
(c) litatunga sheria-
...
(iii) ili kudhibiti utambuzi na ulinzi wa mali ya wana ndoa na hususani nyumba ya wanandoa wakati na siku ya kuvunjika kwa ndoa;
… (Kifungu cha 68)
Marriage and Family Life
Kenya
- English(1) Every child has the right
…
(e) to parental care and protection, which includes equal responsibility of the mother and father to provide for the child, whether they are married to each other or not;
… (Art. 53) - Swahili(1) Kila mtoto ana haki
…
(e) ya malezi na ulinzi wa wazazi, ambayo hujumuisha jukumu sawa la mama na baba kumhudumia mtoto, iwe wameoana au la;
… (Kifungu cha 53)
Marriage and Family Life
Kenya
- English(1) The family is the natural and fundamental unit of society and the necessary basis of social order, and shall enjoy the recognition and protection of the State.
(2) Every adult has the right to marry a person of the opposite sex, based on the free consent of the parties.
(3) Parties to a marriage are entitled to equal rights at the time of the marriage, during the marriage and at the dissolution of the marriage.
(4) Parliament shall enact legislation that recognises—
(a) marriages concluded under any tradition, or system of religious, personal or family law; and
(b) any system of personal and family law under any tradition, or adhered to by persons professing a particular religion, to the extent that any such marriages or systems of law are consistent with this Constitution. (Art. 45) - Swahili(1) Familia ni kiungo cha asili na cha msingi cha jamii na msingi muhimu wa maadili ya kijamii, na itanufaika na kutambuliwa na kulindwa na Serikali.
(2) Kila mtu mzima ana haki ya kuoa mtu wa jinsia tofauti, kwa kuzingatia ridhaa huru ya pande zote.
(3) Pande zote katika ndoa zina haki sawa siku ya ndoa, wakati wa ndoa na wakati wa kuvunja ndoa.
(4) Bunge litatunga sheria inayotambua-
(a) ndoa zilizofungwa chini ya utamaduni wowote, au mfumo wa sheria za kidini, za binafsi au za familia; na
(b) mfumo wowote wa sheria ya binafsi au familia chini ya utamaduni wowote, au inazingatiwa na watu ambao ni waumini wa dini fulani, kwa kiwango kwamba ndoa yoyote ya namna hiyo au mifumo ya sheria haipingani na Katiba hii. (Kifungu cha 45)
Marriage and Family Life
Kenya
- EnglishEvery person has the right to privacy, which includes the right not to have—
…
(c) information relating to their family or private affairs unnecessarily required or revealed;
… (Art. 31) - SwahiliKila mtu ana haki ya faragha, ambayo ni pamoja na haki ya kutokuwa na—
…
(c) habari zinazohusiana na familia zao au mambo yao binafsi yanayotakiwa au kufichuliwa isivyo lazima;
… (Kifungu cha 31)