Constitution of the Republic of Kenya 2010
Indigenous Peoples
  • English

    2. The national values and principles of governance include-

    b. human dignity, equity, social justice, inclusiveness, equality, human rights, non-discrimination and protection of the marginalised;
    … (Art. 10)
  • Swahili

    (2) Tunu za kitaifa na kanuni za utawala ni pamoja na-

    (b) utu wa binadamu, haki, haki ya kijamii, umoja, usawa, haki za binadamu, kutokuwa na ubaguzi na ulinzi kwa waliotengwa na jamii;
    … (Kifungu cha 10)
Indigenous Peoples
  • English
    ...
    (3) All State organs and all public officers have the duty to address the needs of vulnerable groups within society, including women, older members of society, persons with disabilities, children, youth, members of minority or marginalised communities, and members of particular ethnic, religious or cultural communities.
    … (Art. 21)
  • Swahili
    ...
    (3) Vyombo vyote vya Serikali na watumishi wa umma wana wajibu wa kushughulikia mahitaji ya makundi yaliyopo katika mazingira hatarishi katika jamii, ikiwa ni pamoja na wanawake, wazee, watu wenye ulemavu, watoto, vijana, wanajamii wenye uwakilishi mdogo katika jamii au watu waliotengwa na jamii, na watu wa jamii ya kabila, dini au utamaduni fulani.
    … (Kifungu cha 21)
Indigenous Peoples
  • English
    The State shall put in place affirmative action programmes designed to ensure that minorities and marginalised groups—
    (a) participate and are represented in governance and other spheres of life;
    (b) are provided special opportunities in educational and economic fields;
    (c) are provided special opportunities for access to employment;
    (d) develop their cultural values, languages and practices; and
    (e) have reasonable access to water, health services and infrastructure. (Art. 56)
  • Swahili
    Serikali itaweka mipango thabiti ya utekelezaji iliyowekwa ili kuhakikisha kwamba watu wenye uwakilishi mdogo katika jamii na makundi yaliyotengwa na jamii-
    (a) wanashiriki na wanawakilishwa katika utawala na nyanja nyingine za maisha;
    (b) wanapewa fursa maalumu katika nyanja za elimu na uchumi;
    (c) wanapewa fursa maalumu za kupata ajira;
    (d) wanakuza tunu zao za kitamaduni, lugha na desturi; na
    (e) wanaweza kupata maji, huduma za afya na miundombinu. (Kifungu cha 56)
Indigenous Peoples
  • English
    (1) Community land shall vest in and be held by communities identified on the basis of ethnicity, culture or similar community of interest.
    (2) Community land consists of—
    (a) land lawfully registered in the name of group representatives under the provisions of any law;
    (b) land lawfully transferred to a specific community by any process of law;
    (c) any other land declared to be community land by an Act of Parliament; and
    (d) land that is—
    (i) lawfully held, managed or used by specific communities as community forests, grazing areas or shrines;
    (ii) ancestral lands and lands traditionally occupied by hunter-gatherer communities; or
    (iii) lawfully held as trust land by the county governments, but not including any public land held in trust by the county government under Article 62(2).
    … (Art. 63)
  • Swahili
    (1) Ardhi ya jamii itakabidhiwa na kushikiliwa na jamii zinazotambuliwa kwa msingi wa kabila, utamaduni au jamii yenye maslahi yanayofanana.
    (2) Ardhi ya jumuiya inajumuisha—
    (a) ardhi iliyosajiliwa kihalali kwa jina la wawakilishi wa kikundi chini ya masharti ya sheria yoyote;
    (b) ardhi ambayo umilikiwa wake umehamishwa kihalali kwenda kwa jamii mahususi kwa mchakato wowote wa sheria;
    (c) ardhi nyingine yoyote iliyotangazwa kuwa ardhi ya jamii kwa Sheria ya Bunge; na
    (d) ardhi ambayo—
    (i) inashikiliwa kihalali, inayosimamiwa au kutumiwa na jamii mahususi kama misitu ya jamii, maeneo ya malisho au shughuli za kiimani;
    (ii) ardhi za mababu na ardhi ambazo kiutamaduni zilishikiliwa na jamii za wawindaji na waokotaji; au
    (iii) imeshikiliwa kisheria na serikali za kaunti kama ardhi ya amana, lakini haijumuishi ardhi yoyote ya umma inayoshikiliwa na serikali ya kaunti chini ya Kifungu cha 62(2).
    ... (Kifungu cha 63)
Indigenous Peoples
  • English
    1. Every political party shall-

    e. respect the right of all persons to participate in the political process, including minorities and marginalised groups;
    … (Art. 91)
  • Swahili
    1. Kila chama cha siasa-

    e. kitaheshimu haki ya watu wote kushiriki katika mchakato wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na watu wenye uwakilishi mdogo katika jamii na makundi yaliyotengwa na jamii;
    … (Kifungu cha 91)
Indigenous Peoples
  • English
    Parliament shall enact legislation to promote the representation in Parliament of—

    (d) ethnic and other minorities; and
    (e) marginalised communities. (Art. 100)
  • Swahili
    Bunge litatunga sheria ili kuimarisha uwakilishi Bungeni wa—

    (d) kabila na watu wengine wenye uwakilishi mdogo katika jamii; na
    (e) jamii za pembezoni. (Kifungu cha 100)
Indigenous Peoples
  • English
    The objects of the devolution of government are—
    ...
    (d) to recognise the right of communities to manage their own affairs and to further their development;
    (e) to protect and promote the interests and rights of minorities and marginalised communities;
    … (Art. 174)
  • Swahili
    Malengo ya ugatuzi wa serikali ni-
    ...
    (d) kutambua haki ya jamii kusimamia mambo yao wenyewe na kukuza maendeleo yao;
    (e) kulinda na kuimarisha masilahi na haki za watu wenye uwakilishi mdogo katika jamii na jamii za pembezoni;
    … (Kifungu cha 174)
Indigenous Peoples
  • English
    The following principles shall guide all aspects of public finance in the Republic
    ...
    (b) the public finance system shall promote an equitable society, and in particular—

    (iii) expenditure shall promote the equitable development of the country, including by making special provision for marginalised groups and areas;
    … (Art. 201)
  • Swahili
    Kanuni zifuatazo zitaongoza nyanja zote za fedha za umma katika Jamhuri
    ...
    (b) mfumo wa fedha za umma utaimarisha jamii yenye usawa, na hususani-

    (iii) matumizi yataimarisha maendeleo sawa ya nchi, ikiwa ni pamoja na kutunga sheria maalumu kwa ajili ya makundi na maeneo ya pembezoni;
    … (Kifungu cha 201)
Indigenous Peoples
  • English

    (3) The national government may use the Equalisation Fund-

    (b) either directly, or indirectly through conditional grants to counties in which marginalised communities exist.
    … (Art. 204)
  • Swahili

    (3) Serikali ya kitaifa inaweza kutumia Mfuko wa Usawa-

    (b) ama kwa dhahiri, au si kwa dhahiri kupitia ruzuku zenye masharti kwenda kwenye kaunti ambazo kuna jamii za pembezoni.
    … (Kifungu cha 204)
Indigenous Peoples
  • English

    • “marginalised community” means-
    (a) a community that, because of its relatively small population or for any other reason, has been unable to fully participate in the integrated social and economic life of Kenya as a whole;
    (b) a traditional community that, out of a need or desire to preserve its unique culture and identity from assimilation, has remained outside the integrated social and economic life of Kenya as a whole;
    (c) an indigenous community that has retained and maintained a traditional lifestyle and livelihood based on a hunter or gatherer economy; or
    (d) pastoral persons and communities, whether they are-
    (i) nomadic; or
    (ii) a settled community that, because of its relative geographic isolation, has experienced only marginal participation in the integrated social and economic life of Kenya as a whole;
    • “marginalised group” means a group of people who, because of laws or practices before, on, or after the effective date, were or are disadvantaged by discrimination on one or more of the grounds in Article 27 (4);
    … (Art. 260)
  • Swahili

    • “jamii ya pembezoni” humaanisha-
    (a) jamii ambayo, kwa sababu ya idadi ndogo ya watu wake au kwa sababu nyingineyo yoyote, imeshindwa kushiriki kikamilifu katika maisha ya kijamii na kiuchumi ya Kenya kwa ujumla;
    (b) jamii ya jadi ambayo, kutokana na hitaji au shauku ya kuhifadhi utamaduni na utambulisho wake wa kipekee na kitambulisho ili usipotee, imebaki nje ya maisha ya kawaida ya kijamii na kiuchumi ya Kenya kwa ujumla;
    (c) jamii asilia ambayo imeshikilia na kudumisha mtindo wa maisha ya jadi na kujipatia riziki katika uchumi wa uwindaji na uokotaji; au
    (d) watu na jamii ya wafugaji, iwe ni-
    (i) wa kuhamahama; au
    (ii) jamii yenye makazi ya kudumu ambayo, kwa sababu ya kujitenga kwake kijiografia, imeshiriki kidogo sana katika maisha ya pamoja ya kijamii na kiuchumi ya Kenya kwa ujumla;
    "Kikundi cha pembezoni" humaanisha kikundi cha watu ambao, kwa sababu ya sheria au desturi za hapo awali, au baada ya tarehe ya utekelezaji walikuwa au wametengwa, kwa kubaguliwa kwa sababu moja au zaidi zilizopo katika Kifungu cha 27 (4);
    … (Kifungu cha 260)
1

Constitution of the Republic of Kenya 2010 (English). According to Art. 7: "… 2. The official languages of the Republic are Kiswahili and English. …"

2

Constitution of the Republic of Kenya 2010 (Swahili). UN Women in-house translation (2020).

Links to all sites last visited 14 February 2024
3
According to Art. 260: “‘Affirmative action’ includes any measure designed to overcome or ameliorate an inequity or the systemic denial or infringement of a right or fundamental freedom;...”.
4
According to Art. 248: “(2) The commissions are— (a) the Kenya National Human Rights and Equality Commission; (b) the National Land Commission; (c) the Independent Electoral and Boundaries Commission; (d) the Parliamentary Service Commission; (e) the Judicial Service Commission; (f) the Commission on Revenue Allocation; (g) the Public Service Commission; (h) the Salaries and Remuneration Commission; (i) the Teachers Service Commission; and (j) the National Police Service Commission.”
5
According to Art. 260: “‘Affirmative action’ includes any measure designed to overcome or ameliorate an inequity or the systemic denial or infringement of a right or fundamental freedom;...”.
6

7
Chapter 4 on Bill of Rights.
8
According to Art. 260: “‘Affirmative action’ includes any measure designed to overcome or ameliorate an inequity or the systemic denial or infringement of a right or fundamental freedom;...”.
9

10
According to Art. 260: “‘Affirmative action’ includes any measure designed to overcome or ameliorate an inequity or the systemic denial or infringement of a right or fundamental freedom;...”.
11

12
Chapter 4 on Bill of Rights.
13
Chapter 4 on Bill of Rights.