Constitution of the Republic of Kenya 2010
Political Rights and Association
  • English

    (3) Women and men have the right to equal treatment, including the right to equal opportunities in political, economic, cultural and social spheres.
    … (Art. 27)
  • Swahili

    (3) Wanawake na wanaume wana haki ya kutendewa kwa usawa, ikiwa ni pamoja na haki ya kuwa na fursa sawa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.
    … (Kifungu cha27)
Political Rights and Association
  • English
    (1) Every person has the right to freedom of association, which includes the right to form, join or participate in the activities of an association of any kind.
    … (Art. 36)
  • Swahili
    (1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kujumuika, ambayo hujumuisha haki ya kuunda, kujiunga au kushiriki katika shughuli za chama cha aina yoyote.
    … (Kifungu cha 36)
Political Rights and Association
  • English
    (1) Every citizen is free to make political choices, which includes the right—
    (a) to form, or participate in forming, a political party;
    (b) to participate in the activities of, or recruit members for, a political party; or
    (c) to campaign for a political party or cause.
    (2) Every citizen has the right to free, fair and regular elections based on universal suffrage and the free expression of the will of the electors for—
    (a) any elective public body or office established under this Constitution; or
    (b) any office of any political party of which the citizen is a member.
    (3) Every adult citizen has the right, without unreasonable restrictions—
    (a) to be registered as a voter;
    (b) to vote by secret ballot in any election or referendum; and
    (c) to be a candidate for public office, or office within a political party of which the citizen is a member and, if elected, to hold office. (Art. 38)
  • Swahili
    (1) Kila raia yuko huru kufanya chaguzi za kisiasa, ambazo ni pamoja na haki-
    (a) ya kuunda, au kushiriki katika kuunda chama cha siasa;
    (b) kushiriki katika shughuli za, au kuwaandikisha wanachama wa chama cha siasa; au
    (c) kufanyia kampeni chama cha kisiasa au shughuli.
    (2) Kila raia ana haki ya kushiriki chaguzi huru, za haki na za mara kwa mara zenye msingi wa haki majumui ya kupiga kura na uhuru wa kuelezea nia ya wachaguliwa kwa—
    (a) chombo chochote cha kuchaguliwa au ofisi iliyoanzishwa chini ya Katiba hii; au
    (b) ofisi yoyote ya chama chochote cha kisiasa ambacho raia huyo ni mwanachama wake.
    (3) Kila raia mtu mzima ana haki, bila vizuizi visivyo vya msingi-
    (a) ya kuandikishwa kama mpiga kura;
    (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au kura ya maoni; na
    (c) kuwa mtaradhia wa ofisi ya umma, au ofisi ndani ya chama cha siasa ambacho raia huyo ni mwanachama wake na, ikiwa amechaguliwa kushika wadhifa. (Kifungu cha 38)
Political Rights and Association
  • English
    The electoral system shall comply with the following principles—
    (a) freedom of citizens to exercise their political rights under Article 38;
    (b) not more than two-thirds of the members of elective public bodies shall be of the same gender;
    … (Art. 81)
  • Swahili
    Mfumo wa uchaguzi utazingatia kanuni zifuatazo-
    (a) uhuru wa raia kutumia haki yao ya kisiasa chini ya Kifungu cha 38;
    (b) si zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wa vyombo vya umma vya kuchaguliwa watakuwa wa jinsia moja;
    … (Kifungu cha 81)
Political Rights and Association
  • English
    (1) A person qualifies for registration as a voter at elections or referenda if the person—
    (a) is an adult citizen;
    (b) is not declared to be of unsound mind; and
    (c) has not been convicted of an election offence during the preceding five years.
    … (Art. 83)
  • Swahili
    (1) Mtu anastahili kuandikishwa kama mpiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni ikiwa mtu huyo—
    (a) ni raia mtu mzima;
    (b) hajatangazwa kuwa na ugonjwa wa akili; na
    (c) hajakutwa kuwa na kosa la uchaguzi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
    … (Kifungu cha 83)
National level
  • English
    ...
    (6) To give full effect to the realisation of the rights guaranteed under this Article, the State shall take legislative and other measures, including affirmative action10 programmes and policies designed to redress any disadvantage suffered by individuals or groups because of past discrimination.
    (7) Any measure taken under clause (6) shall adequately provide for any benefits to be on the basis of genuine need.
    (8) In addition to the measures contemplated in clause (6), the State shall take legislative and other measures to implement the principle that not more than two-thirds of the members of elective or appointive bodies shall be of the same gender. (Art. 27)
  • Swahili
    ...
    (6) Ili kutekeleza kikamilifu utekelezaji wa haki zilizohakikishwa chini ya IKifungu hiki, Serikali itachukua hatua za kisheria na hatua nyinginezo, pamoja na mipango na sera thabiti za utekelezaji zilizoundwa ili kufidia unyimwaji wa haki ambao uliwapata watu au kikundi cha watu kwa sababu ya ubaguzi wa zamani.
    (7) Hatua yoyote inayochukuliwa chini ya ibara ya (6) itatoa kikamilifu maslahi kwa msingi wa hitaji la kweli.
    (8) Pamoja na hatua zilizobainishwa katika ibara ya (6), Serikali itachukua hatua za kisheria na hatua nyinginezo ili kutekeleza kanuni ambayo itahakikisha kwamba washirika wa bodi wa kuchaguliwa au kuteuliwa wa jinsia moja hawatakuwa zaidi ya theluthi mbili. (Kifungu cha 27)
National level
  • English
    The electoral system shall comply with the following principles

    (b) not more than two-thirds of the members of elective public bodies shall be of the same gender;

    (d) universal suffrage based on the aspiration for fair representation and equality of vote;
    … (Art. 81)
  • Swahili
    Mfumo wa uchaguzi utazingatia kanuni zifuatazo

    (b) si zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wa vyombo vya umma vya kuchaguliwa watakuwa wa jinsia moja;

    (d) haki majumui ya kupiga kura kwa msingi wa matamanio ya uwakilishi wa haki na usawa wa kura;
    … (Kifungu cha 81)
National level
  • English
    (1) Elections for the seats in Parliament provided for under Articles 97(1)(c) and 98(1)(b), (c) and (d), and for the members of county assemblies under article 177(1)(b) and (c), shall be on the basis of proportional representation by use of party lists.
    (2) The Independent Electoral and Boundaries Commission shall be responsible for the conduct and supervision of elections for seats provided for under clause (1) and shall ensure that—

    (b) except in the case of the seats provided for under Article 98(1)(b), each party list comprises the appropriate number of qualified candidates and alternates between male and female candidates in the priority in which they are listed;
    … (Art. 90)
  • Swahili
    (1) Chaguzi wa viti katika Bunge vilivyowekwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c) na 98 (1) (b), (c) na (d), na kwa wajumbe wa mabunge ya kaunti chini ya kifungu cha 177 (1) (b) na (c), zitakuwa kwa msingi wa uwakilishi wa usawa kwa kutumia orodha ya chama.
    (2) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itakuwa na jukumu la kufanya na kusimamia uchaguzi wa viti vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1) na itahakikisha kwamba—

    (b) isipokuwa katika viti vilivyobainishwa chini ya Kifungu cha 98 ( 1)(b), orodha ya kila chama inajumuisha idadi inayofaa ya wagombea wenye sifa na wanabadilishana kati ya wagombea wa kiume na wa kike katika kipaumbele ambacho kwacho wameorodheshwa;
    … (Kifungu cha 90)
National level
  • English
    (1) The National Assembly consists of—

    (b) forty-seven women, each elected by the registered voters of the counties, each county constituting a single member constituency;
    … (Art. 97)
  • Swahili
    (1) Bunge la Kitaifa linajumuisha—

    (b) wanawake arobaini na saba, kila mmoja aliyechaguliwa na wapiga kura wa kaunti, kila kaunti inaunda jimbo moja la uchaguzi;
    … (Kifungu cha 97)
National level
  • English
    (1) The Senate consists of—

    (b) sixteen women members who shall be nominated by political parties according to their proportion of members of the Senate elected under clause (a) in accordance with Article 90;
    (c) two members, being one man and one woman, representing the youth;
    (d) two members, being one man and one woman, representing persons with disabilities;
    … (Art. 98)
  • Swahili
    (1) Bunge la Seneti linajumuisha—
    ...
    (b) wajumbe wanawake kumi na sita watakaoteuliwa na vyama vya siasa kulingana na idadi yao ya wajumbe wa Seneti waliochaguliwa chini ya ibara ya (a) kwa mujibu wa Kifungu cha 90;
    (c) wajumbe wawili, mmoja akiwa mwanaume na mmoja mwanamke, wakiwawakilisha vijana;
    (d) wajumbe wawili, mmoja akiwa mwanaume anayewakilisha watu wenye ulemavu;
    … (Kifungu cha 98)
Subnational levels
  • English
    County governments established under this Constitution shall reflect the following principles

    (c) no more than two-thirds of the members of representative bodies in each county government shall be of the same gender. (Art. 175)
  • Swahili
    Serikali za kaunti zilizoanzishwa chini ya Katiba hii zitaongozwa na kanuni zifuatazo

    (c) hakuna zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wa vyombo vya wawakilishi katika kila serikali ya kaunti watakuwa wa jinsia moja. (Kifungu cha 175)
Subnational levels
  • English
    A county assembly consists of—
    (a) members elected by the registered voters of the wards, each ward constituting a single member constituency, on the same day as a general election of Members of Parliament, being the second Tuesday in August, in every fifth year;
    (b) the number of special seat members necessary to ensure that no more than two-thirds of the membership of the assembly are of the same gender;
    … (Art. 177)
  • Swahili
    Bunge la kaunti linaundwa na -
    (a) wajumbe waliochaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa wa kata, kila kata inaunda jimbo moja la uchaguzi, katika siku iyo hiyo ya uchaguzi mkuu wa Wabunge, itakuwa Jumanne ya pili ya mwezi Agosti, kila baada ya miaka mitano;
    (b) idadi ya wajumbe wa viti maalumu ambayo ni ya lazima ili kuhakikisha kwamba si zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wa bunge hilo wanakuwa wa jinsia moja;
    … (Kifungu cha 177)
Subnational levels
  • English
    (1) Not more than two-thirds of the members of any county assembly or county executive committee shall be of the same gender.
    … (Art. 197)
  • Swahili
    (1) Si zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wa bunge lolote la kaunti au kamati kuu ya kaunti watakuwa wa jinsia moja.
    … (Kifungu cha 197)
Political Parties
  • English
    (1) Elections for the seats in Parliament provided for under Articles 97(1)(c) and 98(1)(b), (c) and (d), and for the members of county assemblies under article 177(1)(b) and (c), shall be on the basis of proportional representation by use of party lists.
    (2) The Independent Electoral and Boundaries Commission shall be responsible for the conduct and supervision of elections for seats provided for under clause (1) and shall ensure that—
    (a) each political party participating in a general election nominates and submits a list of all the persons who would stand elected if the party were to be entitled to all the seats provided for under clause (1), within the time prescribed by national legislation;
    (b) except in the case of the seats provided for under Article 98 (1) (b), each party list comprises the appropriate number of qualified candidates and alternates between male and female candidates in the priority in which they are listed;
    (c) except in the case of county assembly seats, each party list reflects the regional and ethnic diversity of the people of Kenya.
    … (Art. 90)
  • Swahili
    (1) Chaguzi wa viti katika Bunge vilivyowekwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c) na 98 (1) (b), (c) na (d), na kwa wajumbe wa mabunge ya kaunti chini ya kifungu cha 177 (1) (b) na (c), zitakuwa kwa msingi wa uwakilishi wa usawa kwa kutumia orodha ya chama.
    (2) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itakuwa na jukumu la kufanya na kusimamia uchaguzi wa viti vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1) na itahakikisha kwamba—
    (a) kila chama cha siasa kinachoshiriki katika uchaguzi mkuu kinateua na kuwasilisha orodha ya watu wote ambao watasimama kuchaguliwa ikiwa chama kitastahili kupewa viti vyote vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1), ndani ya muda uliowekwa na sheria ya kitaifa;
    (b) isipokuwa kwa viti vilivyobainishwa chini ya Kifungu cha 98 (1) (b), kila orodha ya chama inajumuisha idadi inayofaa ya wagombea wenye sifa na wanabadilishana kati ya wagombea wa kiume na wa kike katika kipaumbele ambacho kwacho wameorodheshwana;
    (c) isipokuwa kwa viti vya bunge la kaunti, kila orodha ya chama inaonyesha uanuwai wa kikanda na kikabila wa watu wa Kenya.
    … (Kifungu cha 90)
Political Parties
  • English
    (1) Every political party shall—
    (a) have a national character as prescribed by an Act of Parliament;
    (b) have a democratically elected governing body;
    (c) promote and uphold national unity;
    (d) abide by the democratic principles of good governance, promote and practise democracy through regular, fair and free elections within the party;
    (e) respect the right of all persons to participate in the political process, including minorities and marginalised groups;
    (f) respect and promote human rights and fundamental freedoms, and gender equality and equity;
    (g) promote the objects and principles of this Constitution and the rule of law; and
    (h) subscribe to and observe the code of conduct for political parties.
    (2) A political party shall not—
    (a) be founded on a religious, linguistic, racial, ethnic, gender or regional basis or seek to engage in advocacy of hatred on any such basis;
    (b) engage in or encourage violence by, or intimidation of, its members, supporters, opponents or any other person;
    (c) establish or maintain a paramilitary force, militia or similar organisation;
    (d) engage in bribery or other forms of corruption; or
    (e) except as is provided under this Chapter or by an Act of Parliament, accept or use public resources to promote its interests or its candidates in elections. (Art. 91)
  • Swahili
    (1) Kila chama cha siasa-
    (a) kitakuwa na sifa ya kitaifa kama ilivyoamriwa na Sheria ya Bunge;
    (b) kitakuwa na chombo cha uongozi kinachochaguliwa kidemokrasia;
    (c) kitaimarisha na kushikilia umoja wa kitaifa;
    (d) kitafungwa na kanuni za kidemokrasia za utawala bora, kuimarisha na kutekeleza demokrasia kupitia chaguzi huru na za haki za mara kwa mara ndani ya chama;
    (e) kuheshimu haki ya watu wote kushiriki katika mchakato wa kisiasa, pamoja na watu wenye uwakilishi mdogo katika jamii na jamii za pembezoni;
    (f) kuheshimu na kuimarisha haki za binadamu na uhuru wa msingi, na usawa wa kijinsia na haki;
    (g) kuimarisha malengo na kanuni za Katiba hii na utawala wa sheria; na (h) kufuatilia na kuzingatia kanuni za maadili kwa vyama vya siasa.
    (2) Chama cha siasa-
    (a) hakitaanzishwa kwa msingi wa kidini, lugha, rangi, kabila, jinsia au kikanda au kutafuta kujihusisha na uenezajii wa chuki kwa msingi wowote wa aina hiyo;
    (b) kujihusisha au kuchochea vurugu kwa, ama kwa kuwatisha wanachama wake, wafuasi, wapinzani au mtu mwingine yeyote;
    (c) kuanzisha au kuendesha kikundi chenye mwonekano wa kijeshi, mgambo au vyombo kama hivyo;
    (d) kujihusisha na rushwa au aina nyingineyo ya ufisadi; au
    (e) isipokuwa kama ilivyoonyeshwa chini ya Sura hii au kwa Sheria ya Bunge, kukubali au kutumia rasilimali za umma kuimarisha masilahi yake au ya wagombea wake katika chaguzi. (Kifungu cha 91)
Electoral Bodies
  • English

    (1) There is established the Independent Electoral and Boundaries Commission.

    (4) The Commission is responsible for conducting or supervising referenda and elections to any elective body or office established by this Constitution, and any other elections as prescribed by an Act of Parliament
    … (Art. 88)

  • Swahili

    (1) Kuna Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka.

    (4) Tume inawajibika katika kufanya au kusimamia kura za maoni na chaguzi kwa chombo chochote kilichochaguliwa au ofisi iliyoanzishwa na Katiba hii, na chaguzi nyingine zozote kama ilivyoainishwa na Sheria ya Bunge
    … (Kifungu cha 88)

Electoral Bodies
  • English
    (1) Elections for the seats in Parliament provided for under Articles 97(1)(c) and 98(1)(b), (c) and (d), and for the members of county assemblies under article 177(1)(b) and (c), shall be on the basis of proportional representation by use of party lists.
    (2) The Independent Electoral and Boundaries Commission shall be responsible for the conduct and supervision of elections for seats provided for under clause (1) and shall ensure that—
    (a) each political party participating in a general election nominates and submits a list of all the persons who would stand elected if the party were to be entitled to all the seats provided for under clause (1), within the time prescribed by national legislation;
    (b) except in the case of the seats provided for under Article 98 (1) (b), each party list comprises the appropriate number of qualified candidates and alternates between male and female candidates in the priority in which they are listed;
    (c) except in the case of county assembly seats, each party list reflects the regional and ethnic diversity of the people of Kenya.
    … (Art. 90)
  • Swahili
    (1) Chaguzi wa viti katika Bunge vilivyowekwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c) na 98 (1) (b), (c) na (d), na kwa wajumbe wa mabunge ya kaunti chini ya kifungu cha 177 (1) (b) na (c), zitakuwa kwa msingi wa uwakilishi wa usawa kwa kutumia orodha ya chama.
    (2) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itakuwa na jukumu la kufanya na kusimamia uchaguzi wa viti vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1) na itahakikisha kwamba—
    (a) kila chama cha siasa kinachoshiriki katika uchaguzi mkuu kinateua na kuwasilisha orodha ya watu wote ambao watasimama kuchaguliwa ikiwa chama kitastahili kupewa viti vyote vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1), ndani ya muda uliowekwa na sheria ya kitaifa;
    (b) isipokuwa kwa viti vilivyobainishwa chini ya Kifungu cha 98 (1) (b), kila orodha ya chama inajumuisha idadi inayofaa ya wagombea wenye sifa na wanaobadilishana kati ya wagombea wa kiume na wa kike katika kipaumbele ambacho kwacho wameorodheshwa;
    (c) isipokuwa kwa viti vya bunge la kaunti, kila orodha ya chama inaonyesha uanuwai wa kikanda na kikabila wa watu wa Kenya.
    … (Kifungu cha 90)
Electoral Bodies
  • English

    (11) The chairperson and vice-chairperson of a commission11 shall not be of the same gender.
    … (Art. 250)
  • Swahili

    (11) Mwenyeketi na makamu mwenyekiti wa tume hawatakuwa wa jinsia moja.
    … (Kifungu cha 250)
Head of State
  • English
    (1) The President—
    (a) is the Head of State and Government;
    (b) exercises the executive authority of the Republic, with the assistance of the Deputy President and Cabinet Secretaries;

    (2) The President shall-
    (a) respect, uphold and safeguard this Constitution;
    ...
    (e) ensure the protection of human rights and fundamental freedoms and the rule of law.
    ... (Art. 131)
  • Swahili
    (1) Rais-
    (a) ni Mkuu wa Nchi na Serikali;
    (b) anatekeleza mamlaka ya juu ya Jamhuri, kwa kusaidiwa na Makamu wa Rais na Makatibu wa Baraza la Mawaziri;

    (2) Rais-
    (a) ataheshimu, kuitetea na kuilinda Katiba hii;
    ...
    (e) atahakikisha ulinzi wa haki za binadamu na uhuru wa msingi na utawala wa sheria.
    ... (Kifungu cha 131)
Head of State
  • English
    (1) The President shall be elected by registered voters in a national election conducted in accordance with this Constitution and any Act of Parliament regulating presidential elections.
    … (Art. 136)
  • Swahili
    (1) Rais atachaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa katika uchaguzi wa kitaifa unaofanywa kwa mujibu wa Katiba hii na Sheria yoyote ya Bunge inayosimamia uchaguzi wa rais.
    … (Kifungu cha 136)
Head of State
  • English
    (1) A person qualifies for nomination as a presidential candidate if the person—
    (a) is a citizen by birth;
    (b) is qualified to stand for election as a member of Parliament;
    (c) is nominated by a political party, or is an independent candidate; and
    (d) is nominated by not fewer than two thousand voters from each of a majority of the counties.
    … (Art. 137)
  • Swahili
    (1) Mtu anakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa mgombea wa urais ikiwa mtu huyo—
    (a) ni raia kwa kuzaliwa;
    (b) ana sifa za kusimama kwenye uchaguzi kama mbunge;
    (c) ameteuliwa na chama cha siasa, au ni mgombea wa kujitegemea; na
    (d) ameteuliwa na si chini ya wapiga kura elfu mbili kutoka kila kaunti yenye watu wengi.
    … (Kifungu cha 137)
Vice-President
  • English
    (1) The Deputy President shall be the principal assistant of the President and shall deputise for the President in the execution of the President’s functions.
    (2) The Deputy President shall perform the functions conferred by this Constitution and any other functions of the President as the President may assign.
    (3) Subject to Article 134, when the President is absent or is temporarily incapacitated, and during any other period that the President decides, the Deputy President shall act as the President.
    … (Art. 147)
  • Swahili
    (1) Makamu wa Rais atakuwa msaidizi mkuu wa Rais na atamwakilisha Rais katika utekelezaji wa shughuli za Rais.
    (2) Makamu wa Rais atafanya majukumu yaliyoainishwa na Katiba hii na majukumu mengine yoyote ya Rais kadri Rais atakavyompatia.
    (3) Kwa kuzingatia Kifungu cha 134, Rais asipokuwepo au hawezi kufanya kazi kwa muda, na katika kipindi kingine chochote ambacho Rais ataamua, Makamu wa Rais atafanya kazi kama Rais.
    … (Kifungu cha 147)
Vice-President
  • English
    (1) Each candidate in a presidential election shall nominate a person who is qualified for nomination for election as President, as a candidate for Deputy President.
    (2) For the purposes of clause (1), there shall be no separate nomination process for the Deputy President and Article 137 (1) (d) shall not apply to a candidate for Deputy President.
    (3) The Independent Electoral and Boundaries Commission shall declare the candidate nominated by the person who is elected as the President to be elected as the Deputy President.
    … (Art. 148)
  • Swahili
    (1) Kila mgombea katika uchaguzi wa rais atamteua mtu mwenye sifa za kuchaguliwa kuwa Rais, kuwa mtaradhia wa Makamu wa Rais.
    (2) Kwa madhumuni ya ibara ya (1), hakutakuwa na mchakato tofauti wa uteuzi wa Makamu wa Rais na Kifungu cha 137 (1) (d) hakitatumika kwa mtaradhia wa Makamu wa Rais.
    (3) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itamtangaza mtaradhia aliyeteuliwa na mtu aliyechaguliwa kuwa Rais kuchaguliwa kama Makamu wa Rais.
    … (Kifungu cha 148)
Government
  • English
    (1) The national executive of the Republic comprises the President, the Deputy President and the rest of the Cabinet.
    (2) The composition of the national executive shall reflect the regional and ethnic diversity of the people of Kenya. (Art. 130)
  • Swahili
    (1) Serikali kuu ya Jamhuri inaundwa na Rais, Makamu wa Rais na Baraza la Mawaziri.
    (2) Muundo wa serikali kuu ya kitaifa utaakisi umajumui wa kikanda na kikabila wa watu wa Kenya. (Kifungu cha 130)
Government
  • English
    (1) The Cabinet consists of—
    (a) the President;
    (b) the Deputy President;
    (c) the Attorney-General; and
    (d) not fewer than fourteen and not more than twenty-two Cabinet Secretaries.
    (2) The President shall nominate and, with the approval of the National Assembly, appoint Cabinet Secretaries.
    … (Art. 152)
  • Swahili
    (1) Baraza la Mawaziri linaundwa na—
    (a) Rais;
    (b) Makamu wa Rais;
    (c) Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na
    (d) si chini ya Makatibu wa Baraza la Mawaziri kumi na wanne na si zaidi ya ishirini na wawili.
    (2) Rais atapendekeza na, kwa idhini ya Bunge la Kitaifa, atawateua Makatibu wa Baraza la Mawaziri.
    … (Kifungu cha 152)
Legislature
  • English
    (1) Elections for the seats in Parliament provided for under Articles 97(1) (c) and 98 (1) (b), (c) and (d), and for the members of county assemblies under 177 (1) (b) and (c), shall be on the basis of proportional representation by use of party lists.
    (2) The Independent Electoral and Boundaries Commission shall be responsible for the conduct and supervision of elections for seats provided for under clause (1) and shall ensure that—

    (b) except in the case of the seats provided for under Article 98 (1) (b), each party list comprises the appropriate number of qualified candidates and alternates between male and female candidates in the priority in which they are listed;
    … (Art. 90)
  • Swahili
    (1) Uchaguzi wa viti katika Bunge vilivyobainishwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c) na 98 (1) (b), (c) na (d), na kwa wajumbe wa mabunge ya kaunti chini ya kifungu cha 177 (1) (b) na (c), zitakuwa kwa msingi wa uwakilishi wa usawa kwa kutumia orodha za chama.
    (2) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itakuwa na jukumu la kufanya na kusimamia uchaguzi wa viti vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1) na itahakikisha kwamba—

    (b) isipokuwa katika viti vilivyobainishwa chini ya Kifungu cha 98 ( 1)(b), orodha ya kila chama inajumuisha idadi inayofaa ya wagombea wenye sifa na wanabadilishana kati ya wagombea wa kiume na wa kike katika kipaumbele ambacho kwacho wameorodheshwa;
    … (Kifungu cha 90)
Legislature
  • English
    (1) There is established a Parliament of Kenya, which shall consist of the National Assembly and the Senate.
    (2) The National Assembly and the Senate shall perform their respective functions in accordance with this Constitution. (Art. 93)
  • Swahili
    (1) Kuna Bunge la Kenya, ambalo litaundwa na Bunge la Kitaifa na Seneti.
    (2) Vyombo vya Bunge la Kitaifa na Seneti vitafanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba hii. (Kifungu cha 93)
Legislature
  • English
    1. The legislative authority of the Republic is derived from the people and, at the national level, is vested in and exercised by Parliament.
    … (Art. 94)
  • Swahili
    1. Mamlaka ya kisheria ya Jamhuri yanatoka kwa watu na, kwa kiwango cha kitaifa, yanakabidhiwa na kutekelezwa na Bunge.
    … (Kifungu cha 94)
Legislature
  • English
    (1) The National Assembly consists of—
    (a) two hundred and ninety members, each elected by the registered voters of single member constituencies;
    (b) forty-seven women, each elected by the registered voters of the counties, each county constituting a single member constituency;
    (c) twelve members nominated by parliamentary political parties according to their proportion of members of the National Assembly in accordance with Article 90, to represent special interests including the youth, persons with disabilities and workers; and
    (d) the Speaker, who is an ex officio member.
    (2) Nothing in this Article shall be construed as excluding any person from contesting an election under clause (1) (a). (Art. 97)
  • Swahili
    (1) Bunge la Kitaifa linaundwa na—
    (a) wabunge mia mbili na tisini, kila mmoja aliyechaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa kutoka katika eneo bunge moja;
    (b) wanawake arobaini na saba, kila mmoja aliyechaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa wa kaunti, kila kaunti inaunda eneo bunge moja;
    (c) wajumbe kumi na wawili walioteuliwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni kulingana na idadi yao ya wajumbe wa Bunge la Kitaifa kwa mujibu wa Kifungu cha 90, ili kuwakilisha masilahi maalumu ikiwa ni pamoja na vijana, watu wenye ulemavu na wafanyikazi; na
    (d) Spika, ambaye ni mjumbe kwa nafasi yake.
    (2) Hakuna chochote katika Kifungu hiki kitachukuliwa kama kumwondoa mtu yeyote kugombea kwenye uchaguzi chini ya ibara ya (1) (a). (Kifungu cha 97)
Legislature
  • English
    (1) The Senate consists of—
    (a) forty-seven members each elected by the registered voters of the counties, each county constituting a single member constituency;
    (b) sixteen women members who shall be nominated by political parties according to their proportion of members of the Senate elected under clause (a) in accordance with Article 90;
    (c) two members, being one man and one woman, representing the youth;
    (d) two members, being one man and one woman, representing persons with disabilities; and
    (e) the Speaker, who shall be an ex officio member.
    (2) The members referred to in clause (1) (c) and (d) shall be elected in accordance with Article 90.
    (3) Nothing in this Article shall be construed as excluding any person from contesting an election under clause (1) (a). (Art. 98)
  • Swahili
    (1) Bunge la Seneti linaundwa na -
    (a) wajumbe arobaini na saba kila mmoja aliyechaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa wa kaunti husika, kila kaunti inaunda eneo bunge moja;
    (b) wajumbe wanawake kumi na sita ambao watachaguliwa na vyama vya siasa kulingana na idadi yao ya wajumbe wa Seneti waliochaguliwa chini ya ibara ya (a) kwa mujibu wa Kifungu cha 90;
    (c) wajumbe wawili, mmoja akiwa mwanaume na mwingine mwanamke wakiwakilisha vijana;
    (d) wajumbe wawili, mmoja akiwa mwanaume na mwingine mwanamke wakiwakilisha watu wenye ulemavu; na
    (e) Spika, ambaye atakuwa mjumbe kwa nafasi yake.
    (2) Wajumbe waliotajwa katika ibara ya (1) (c) na (d) watachaguliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 90.
    (3) Hakuna chochote katika Kifungu hiki kitachukuliwa kama kumwondoa mtu yeyote kugombea kwenye uchaguzi chini ya ibara ya (1) (a). (Kifungu cha 98)
Legislature
  • English
    (1) Unless disqualified under clause (2), a person is eligible for election as a member of Parliament if the person—
    (a) is registered as a voter;
    (b) satisfies any educational, moral and ethical requirements prescribed by this Constitution or by an Act of Parliament; and
    (c) is nominated by a political party, or is an independent candidate who is supported—
    (i) in the case of election to the National Assembly, by at least one thousand registered voters in the constituency; or
    (ii) in the case of election to the Senate, by at least two thousand registered voters in the county.
    … (Art. 99)
  • Swahili
    (1) Isipokuwa kama hana sifa chini ya ibara ya (2), mtu anastahili kuchaguliwa kama mbunge ikiwa mtu huyo—
    (a) ameandikishwa kama mpiga kura;
    (b) anakidhi matakwa yoyote ya kielimu, ya kiadili na kimaadili yaliyowekwa na Katiba hii au na Sheria ya Bunge; na
    (c) ameteuliwa na chama cha siasa, au ni mgombea huru anayeungwa mkono—
    (i) katika suala la uchaguzi wa Bunge la Kitaifa na wapiga kura angalau elfu moja walioandikishwa katika jimbo hilo la uchaguzi; au
    (ii) katika suala la uchaguzi wa Seneti, na angalau wapiga kura elfu mbili walioandikishwa katika kaunti husika.
    … (Kifungu cha 99)
Legislature
  • English
    Parliament shall enact legislation to promote the representation in Parliament of—
    (a) women;
    (b) persons with disabilities;
    (c) youth;
    (d) ethnic and other minorities; and
    (e) marginalised communities. (Art. 100)
  • Swahili
    Bunge litatunga sheria ili kuimarisha uwakilishi Bungeni wa—
    (a) wanawake;
    (b) watu wenye ulemavu;
    (c) vijana;
    (d) kabila na watu wengine wenye uwakilishi mdogo katika jamii; na
    (e) jamii zilizotengwa. (Kifungu cha 100)
1

Constitution of the Republic of Kenya 2010 (English). According to Art. 7: "… 2. The official languages of the Republic are Kiswahili and English. …"

2

Constitution of the Republic of Kenya 2010 (Swahili). UN Women in-house translation (2020).

Links to all sites last visited 14 February 2024
3
According to Art. 260: “‘Affirmative action’ includes any measure designed to overcome or ameliorate an inequity or the systemic denial or infringement of a right or fundamental freedom;...”.
4
According to Art. 248: “(2) The commissions are— (a) the Kenya National Human Rights and Equality Commission; (b) the National Land Commission; (c) the Independent Electoral and Boundaries Commission; (d) the Parliamentary Service Commission; (e) the Judicial Service Commission; (f) the Commission on Revenue Allocation; (g) the Public Service Commission; (h) the Salaries and Remuneration Commission; (i) the Teachers Service Commission; and (j) the National Police Service Commission.”
5
According to Art. 260: “‘Affirmative action’ includes any measure designed to overcome or ameliorate an inequity or the systemic denial or infringement of a right or fundamental freedom;...”.
6

7
Chapter 4 on Bill of Rights.
8
According to Art. 260: “‘Affirmative action’ includes any measure designed to overcome or ameliorate an inequity or the systemic denial or infringement of a right or fundamental freedom;...”.
9

10
According to Art. 260: “‘Affirmative action’ includes any measure designed to overcome or ameliorate an inequity or the systemic denial or infringement of a right or fundamental freedom;...”.
11

12
Chapter 4 on Bill of Rights.
13
Chapter 4 on Bill of Rights.