SEARCH DATABASE
The Global Gender Equality Constitutional Database is a repository of gender equality related provisions in 194 constitutions from around the world. The Database was updated in partnership with the International Bar Association's Human Rights Institute (IBAHRI) and with support from the Swedish International Development Agency (SIDA) and the Government of Japan. Experience its wealth and depth of information by starting your search now.
ABOUT 4 RESULTS
Affirmative Action (Broadly)
Kenya
- EnglishParliament shall enact legislation to promote the representation in Parliament of—
(a) women;
(b) persons with disabilities;
(c) youth;
(d) ethnic and other minorities; and
(e) marginalised communities. (Art. 100) - SwahiliBunge litatunga sheria ili kuimarisha uwakilishi Bungeni wa—
(a) wanawake;
(b) watu wenye ulemavu;
(c) vijana;
(d) kabila na watu wengine wenye uwakilishi mdogo katika jamii; na
(e) jamii zilizotengwa. (Kifungu cha 100)
Affirmative Action (Broadly)
Kenya
- English(1) Every person is equal before the law and has the right to equal protection and equal benefit of the law.
(2) Equality includes the full and equal enjoyment of all rights and fundamental freedoms.
(3) Women and men have the right to equal treatment, including the right to equal opportunities in political, economic, cultural and social spheres.
(4) The State shall not discriminate directly or indirectly against any person on any ground, including race, sex, pregnancy, marital status, health status, ethnic or social origin, colour, age, disability, religion, conscience, belief, culture, dress, language or birth.
(5) A person shall not discriminate directly or indirectly against another person on any of the grounds specified or contemplated in clause (4).
(6) To give full effect to the realisation of the rights guaranteed under this Article, the State shall take legislative and other measures, including affirmative action3 programmes and policies designed to redress any disadvantage suffered by individuals or groups because of past discrimination.
(7) Any measure taken under clause (6) shall adequately provide for any benefits to be on the basis of genuine need.
(8) In addition to the measures contemplated in clause (6), the State shall take legislative and other measures to implement the principle that not more than two-thirds of the members of elective or appointive bodies shall be of the same gender. (Art. 27) - Swahili(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
(2) Haki sawa ni pamoja na kurufahia kikamilifu na kwa usawa haki zote na uhuru wa msingi.
(3) Wanawake na wanaume wana haki ya kutendewa kwa usawa, ikiwa ni pamoja na haki ya kuwa na fursa sawa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.
(4) Serikali haitambagua mtu yeyote kwa dhahiri au si kwa dhahiri kwa msingi wowote ikiwa ni pamoja na mbari, jinsi, mimba, hali ya ndoa, hali ya afya, asili ya kikabila au kijamii, rangi, umri, ulemavu, dini, dhamiri, imani, utamaduni, mavazi, lugha au kuzaliwa.
(5) Mtu yeyote hatambagua mtu yeyote kwa dhahiri ama si kwa dhahiri kwa misingi yoyote iliyobaisnishwa katika ibara ya (4).
(6) Ili kutekeleza kikamilifu utekelezaji wa haki zilizohakikishwa chini ya Ibara hii, Serikali itachukua hatua za kisheria na hatua nyinginezo, pamoja na mipango na sera thabiti za utekelezaji zilizoundwa ili kufidia unyimwaji wa haki ambao uliwapata watu au kikundi cha watu kwa sababu ya ubaguzi wa zamani.
(7) Hatua yoyote inayochukuliwa chini ya ibara ya (6) itatoa kikamilifu maslahi kwa msingi wa hitaji la kweli.
(8) Pamoja na hatua zilizobainishwa katika ibara ya (6), Serikali itachukua hatua za kisheria na hatua nyinginezo ili kutekeleza kanuni ambayo itahakikisha kwamba washirika wa bodi wa kuchaguliwa au kuteuliwa wa jinsia moja hawatakuwa zaidi ya theluthi mbili. (Kifungu cha 27)
Affirmative Action (Broadly)
Kenya
- English…
(11) The chairperson and vice-chairperson of a commission4 shall not be of the same gender.
… (Art. 250) - Swahili…
(11) Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa tume hawatakuwa wa jinsia moja.
… (Kifungu cha 250)
Affirmative Action (Broadly)
Kenya
- English(1) The Judicial Service Commission shall promote and facilitate the independence and accountability of the judiciary and the efficient, effective and transparent administration of justice …
(2) In the performance of its functions, the Commission shall be guided by the following—
...
(b) the promotion of gender equality. (Art. 172) - Swahili(1) Tume ya Huduma ya Mahakama itakuza na kuwezesha uhuru na uwajibikaji wa mahakama na usimamizi wa haki wenye ufanisi na wenye matokeo yanayotarajiwa na wa uwazi ...
(2) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume itaongozwa na mambo yafuatayo—
...
(b) uimarishaji wa usawa wa kijinsia. (Kifungu cha 172)