SEARCH DATABASE
The Global Gender Equality Constitutional Database is a repository of gender equality related provisions in 194 constitutions from around the world. The Database was updated in partnership with the International Bar Association's Human Rights Institute (IBAHRI) and with support from the Swedish International Development Agency (SIDA) and the Government of Japan. Experience its wealth and depth of information by starting your search now.
Political Rights and Association
- English…
(3) Women and men have the right to equal treatment, including the right to equal opportunities in political, economic, cultural and social spheres.
… (Art. 27) - Swahili…
(3) Wanawake na wanaume wana haki ya kutendewa kwa usawa, ikiwa ni pamoja na haki ya kuwa na fursa sawa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.
… (Kifungu cha27)
Political Rights and Association
- English(1) A person qualifies for registration as a voter at elections or referenda if the person—
(a) is an adult citizen;
(b) is not declared to be of unsound mind; and
(c) has not been convicted of an election offence during the preceding five years.
… (Art. 83) - Swahili(1) Mtu anastahili kuandikishwa kama mpiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni ikiwa mtu huyo—
(a) ni raia mtu mzima;
(b) hajatangazwa kuwa na ugonjwa wa akili; na
(c) hajakutwa kuwa na kosa la uchaguzi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
… (Kifungu cha 83)
Political Rights and Association
- EnglishThe electoral system shall comply with the following principles—
(a) freedom of citizens to exercise their political rights under Article 38;
(b) not more than two-thirds of the members of elective public bodies shall be of the same gender;
… (Art. 81) - SwahiliMfumo wa uchaguzi utazingatia kanuni zifuatazo-
(a) uhuru wa raia kutumia haki yao ya kisiasa chini ya Kifungu cha 38;
(b) si zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wa vyombo vya umma vya kuchaguliwa watakuwa wa jinsia moja;
… (Kifungu cha 81)
Political Rights and Association
- English(1) Every citizen is free to make political choices, which includes the right—
(a) to form, or participate in forming, a political party;
(b) to participate in the activities of, or recruit members for, a political party; or
(c) to campaign for a political party or cause.
(2) Every citizen has the right to free, fair and regular elections based on universal suffrage and the free expression of the will of the electors for—
(a) any elective public body or office established under this Constitution; or
(b) any office of any political party of which the citizen is a member.
(3) Every adult citizen has the right, without unreasonable restrictions—
(a) to be registered as a voter;
(b) to vote by secret ballot in any election or referendum; and
(c) to be a candidate for public office, or office within a political party of which the citizen is a member and, if elected, to hold office. (Art. 38) - Swahili(1) Kila raia yuko huru kufanya chaguzi za kisiasa, ambazo ni pamoja na haki-
(a) ya kuunda, au kushiriki katika kuunda chama cha siasa;
(b) kushiriki katika shughuli za, au kuwaandikisha wanachama wa chama cha siasa; au
(c) kufanyia kampeni chama cha kisiasa au shughuli.
(2) Kila raia ana haki ya kushiriki chaguzi huru, za haki na za mara kwa mara zenye msingi wa haki majumui ya kupiga kura na uhuru wa kuelezea nia ya wachaguliwa kwa—
(a) chombo chochote cha kuchaguliwa au ofisi iliyoanzishwa chini ya Katiba hii; au
(b) ofisi yoyote ya chama chochote cha kisiasa ambacho raia huyo ni mwanachama wake.
(3) Kila raia mtu mzima ana haki, bila vizuizi visivyo vya msingi-
(a) ya kuandikishwa kama mpiga kura;
(b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au kura ya maoni; na
(c) kuwa mtaradhia wa ofisi ya umma, au ofisi ndani ya chama cha siasa ambacho raia huyo ni mwanachama wake na, ikiwa amechaguliwa kushika wadhifa. (Kifungu cha 38)
Political Rights and Association
- English(1) Every person has the right to freedom of association, which includes the right to form, join or participate in the activities of an association of any kind.
… (Art. 36) - Swahili(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kujumuika, ambayo hujumuisha haki ya kuunda, kujiunga au kushiriki katika shughuli za chama cha aina yoyote.
… (Kifungu cha 36)
Political Parties
- English(1) Every political party shall—
(a) have a national character as prescribed by an Act of Parliament;
(b) have a democratically elected governing body;
(c) promote and uphold national unity;
(d) abide by the democratic principles of good governance, promote and practise democracy through regular, fair and free elections within the party;
(e) respect the right of all persons to participate in the political process, including minorities and marginalised groups;
(f) respect and promote human rights and fundamental freedoms, and gender equality and equity;
(g) promote the objects and principles of this Constitution and the rule of law; and
(h) subscribe to and observe the code of conduct for political parties.
(2) A political party shall not—
(a) be founded on a religious, linguistic, racial, ethnic, gender or regional basis or seek to engage in advocacy of hatred on any such basis;
(b) engage in or encourage violence by, or intimidation of, its members, supporters, opponents or any other person;
(c) establish or maintain a paramilitary force, militia or similar organisation;
(d) engage in bribery or other forms of corruption; or
(e) except as is provided under this Chapter or by an Act of Parliament, accept or use public resources to promote its interests or its candidates in elections. (Art. 91) - Swahili(1) Kila chama cha siasa-
(a) kitakuwa na sifa ya kitaifa kama ilivyoamriwa na Sheria ya Bunge;
(b) kitakuwa na chombo cha uongozi kinachochaguliwa kidemokrasia;
(c) kitaimarisha na kushikilia umoja wa kitaifa;
(d) kitafungwa na kanuni za kidemokrasia za utawala bora, kuimarisha na kutekeleza demokrasia kupitia chaguzi huru na za haki za mara kwa mara ndani ya chama;
(e) kuheshimu haki ya watu wote kushiriki katika mchakato wa kisiasa, pamoja na watu wenye uwakilishi mdogo katika jamii na jamii za pembezoni;
(f) kuheshimu na kuimarisha haki za binadamu na uhuru wa msingi, na usawa wa kijinsia na haki;
(g) kuimarisha malengo na kanuni za Katiba hii na utawala wa sheria; na (h) kufuatilia na kuzingatia kanuni za maadili kwa vyama vya siasa.
(2) Chama cha siasa-
(a) hakitaanzishwa kwa msingi wa kidini, lugha, rangi, kabila, jinsia au kikanda au kutafuta kujihusisha na uenezajii wa chuki kwa msingi wowote wa aina hiyo;
(b) kujihusisha au kuchochea vurugu kwa, ama kwa kuwatisha wanachama wake, wafuasi, wapinzani au mtu mwingine yeyote;
(c) kuanzisha au kuendesha kikundi chenye mwonekano wa kijeshi, mgambo au vyombo kama hivyo;
(d) kujihusisha na rushwa au aina nyingineyo ya ufisadi; au
(e) isipokuwa kama ilivyoonyeshwa chini ya Sura hii au kwa Sheria ya Bunge, kukubali au kutumia rasilimali za umma kuimarisha masilahi yake au ya wagombea wake katika chaguzi. (Kifungu cha 91)
Political Parties
- English(1) Elections for the seats in Parliament provided for under Articles 97(1)(c) and 98(1)(b), (c) and (d), and for the members of county assemblies under article 177(1)(b) and (c), shall be on the basis of proportional representation by use of party lists.
(2) The Independent Electoral and Boundaries Commission shall be responsible for the conduct and supervision of elections for seats provided for under clause (1) and shall ensure that—
(a) each political party participating in a general election nominates and submits a list of all the persons who would stand elected if the party were to be entitled to all the seats provided for under clause (1), within the time prescribed by national legislation;
(b) except in the case of the seats provided for under Article 98 (1) (b), each party list comprises the appropriate number of qualified candidates and alternates between male and female candidates in the priority in which they are listed;
(c) except in the case of county assembly seats, each party list reflects the regional and ethnic diversity of the people of Kenya.
… (Art. 90) - Swahili(1) Chaguzi wa viti katika Bunge vilivyowekwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c) na 98 (1) (b), (c) na (d), na kwa wajumbe wa mabunge ya kaunti chini ya kifungu cha 177 (1) (b) na (c), zitakuwa kwa msingi wa uwakilishi wa usawa kwa kutumia orodha ya chama.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itakuwa na jukumu la kufanya na kusimamia uchaguzi wa viti vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1) na itahakikisha kwamba—
(a) kila chama cha siasa kinachoshiriki katika uchaguzi mkuu kinateua na kuwasilisha orodha ya watu wote ambao watasimama kuchaguliwa ikiwa chama kitastahili kupewa viti vyote vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1), ndani ya muda uliowekwa na sheria ya kitaifa;
(b) isipokuwa kwa viti vilivyobainishwa chini ya Kifungu cha 98 (1) (b), kila orodha ya chama inajumuisha idadi inayofaa ya wagombea wenye sifa na wanabadilishana kati ya wagombea wa kiume na wa kike katika kipaumbele ambacho kwacho wameorodheshwana;
(c) isipokuwa kwa viti vya bunge la kaunti, kila orodha ya chama inaonyesha uanuwai wa kikanda na kikabila wa watu wa Kenya.
… (Kifungu cha 90)
Electoral Bodies
- English(1) Elections for the seats in Parliament provided for under Articles 97(1)(c) and 98(1)(b), (c) and (d), and for the members of county assemblies under article 177(1)(b) and (c), shall be on the basis of proportional representation by use of party lists.
(2) The Independent Electoral and Boundaries Commission shall be responsible for the conduct and supervision of elections for seats provided for under clause (1) and shall ensure that—
(a) each political party participating in a general election nominates and submits a list of all the persons who would stand elected if the party were to be entitled to all the seats provided for under clause (1), within the time prescribed by national legislation;
(b) except in the case of the seats provided for under Article 98 (1) (b), each party list comprises the appropriate number of qualified candidates and alternates between male and female candidates in the priority in which they are listed;
(c) except in the case of county assembly seats, each party list reflects the regional and ethnic diversity of the people of Kenya.
… (Art. 90) - Swahili(1) Chaguzi wa viti katika Bunge vilivyowekwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c) na 98 (1) (b), (c) na (d), na kwa wajumbe wa mabunge ya kaunti chini ya kifungu cha 177 (1) (b) na (c), zitakuwa kwa msingi wa uwakilishi wa usawa kwa kutumia orodha ya chama.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itakuwa na jukumu la kufanya na kusimamia uchaguzi wa viti vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1) na itahakikisha kwamba—
(a) kila chama cha siasa kinachoshiriki katika uchaguzi mkuu kinateua na kuwasilisha orodha ya watu wote ambao watasimama kuchaguliwa ikiwa chama kitastahili kupewa viti vyote vilivyobainishwa chini ya ibara ya (1), ndani ya muda uliowekwa na sheria ya kitaifa;
(b) isipokuwa kwa viti vilivyobainishwa chini ya Kifungu cha 98 (1) (b), kila orodha ya chama inajumuisha idadi inayofaa ya wagombea wenye sifa na wanaobadilishana kati ya wagombea wa kiume na wa kike katika kipaumbele ambacho kwacho wameorodheshwa;
(c) isipokuwa kwa viti vya bunge la kaunti, kila orodha ya chama inaonyesha uanuwai wa kikanda na kikabila wa watu wa Kenya.
… (Kifungu cha 90)
Electoral Bodies
- English
(1) There is established the Independent Electoral and Boundaries Commission.
…
(4) The Commission is responsible for conducting or supervising referenda and elections to any elective body or office established by this Constitution, and any other elections as prescribed by an Act of Parliament
… (Art. 88) - Swahili
(1) Kuna Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka.
…
(4) Tume inawajibika katika kufanya au kusimamia kura za maoni na chaguzi kwa chombo chochote kilichochaguliwa au ofisi iliyoanzishwa na Katiba hii, na chaguzi nyingine zozote kama ilivyoainishwa na Sheria ya Bunge
… (Kifungu cha 88)
Electoral Bodies
- English…
(11) The chairperson and vice-chairperson of a commission11 shall not be of the same gender.
… (Art. 250) - Swahili…
(11) Mwenyeketi na makamu mwenyekiti wa tume hawatakuwa wa jinsia moja.
… (Kifungu cha 250)