SEARCH DATABASE
The Global Gender Equality Constitutional Database is a repository of gender equality related provisions in 194 constitutions from around the world. The Database was updated in partnership with the International Bar Association's Human Rights Institute (IBAHRI) and with support from the Swedish International Development Agency (SIDA) and the Government of Japan. Experience its wealth and depth of information by starting your search now.
ABOUT 143 RESULTS
Property, Inheritance and Land Tenure
Kenya
- English(1) Land in Kenya shall be held, used and managed in a manner that is equitable, efficient, productive and sustainable, and in accordance with the following principles—
(a) equitable access to land;
(b) security of land rights;
…
(f) elimination of gender discrimination in law, customs and practices related to land and property in land; and
(g) encouragement of communities to settle land disputes through recognised local community initiatives consistent with this Constitution.
(2) These principles shall be implemented through a national land policy developed and reviewed regularly by the national government and through legislation. (Art. 60) - Swahili(1) Ardhi nchini Kenya itashikiliwa, kutumiwa na kusimamiwa kwa namna ambayo ni ya usawa, fanisi, yenye tija na endelevu, na kwa kufuata kanuni zifuatazo-
(a) haki sawa ya kupata ardhi;
(b) amana ya haki za ardhi;
…
(f) kuondoa ubaguzi wa kijinsia katika sheria, mila na desturi zinazohusiana na ardhi na mali katika ardhi; na
(g) kuwahimiza jamii kumaliza migogoro ya ardhi kupitia hatua zinazochukuliwa na jamii bila kukiuka Katiba hii.
(2) Kanuni hizi zitatekelezwa kupitia sera ya ardhi ya kitaifa iliyoundwa na kupitiwa mara kwa mara na serikali ya kitaifa na kupitia sheria. (Kifungu cha 60)
Property, Inheritance and Land Tenure
Kenya
- English...
(5) The jurisdiction of a Kadhis’ court shall be limited to the determination of questions of Muslim law relating to personal status, marriage, divorce or inheritance in proceedings in which all the parties profess the Muslim religion and submit to the jurisdiction of the Kadhi’s courts.
… (Art. 170) - Swahili...
(5) Mamlaka ya Mahakama ya Kadhi yatakuwa na mipaka itakayoishia katika kuamua shauri la sheria ya Kiisilamu inayohusiana na hadhi binafsi, ndoa, talaka au urithi katika kesi ambazo kwazo pande zote ni waumini wa dini ya Kiislamu na wanaitii mamlaka ya mahakama za Kadhi.
… (Kifungu cha 170)
Property, Inheritance and Land Tenure
Kenya
- English(1) Subject to Article 65, every person has the right, either individually or in association with others, to acquire and own property—
(a) of any description; and
(b) in any part of Kenya.
… (Art. 40) - Swahili(1) Kwa kuzingatia Kifungu cha 65, kila mtu ana haki, ama mtu mmoja mmoja au ushirika pamoja na wengine, ya kupata na kumiliki mali-
(a) ya namna yoyote; na
(b) katika sehemu yoyote ya Kenya.
… (Kifungu cha 40)
Property, Inheritance and Land Tenure
Kenya
- EnglishParliament shall—
(a) revise, consolidate and rationalise existing land laws;
(b) revise sectoral land use laws in accordance with the principles set out in Article 60 (1); and
(c) enact legislation—
(i) to prescribe minimum and maximum land holding acreages in respect of private land;
(ii) to regulate the manner in which any land may be converted from one category to another;
(iii) to regulate the recognition and protection of matrimonial property and in particular the matrimonial home during and on the termination of marriage;
(iv) to protect, conserve and provide access to all public land;
(v) to enable the review of all grants or dispositions of public land to establish their propriety or legality;
(vi) to protect the dependants of deceased persons holding interests in any land, including the interests of spouses in actual occupation of land;
… (Art. 68) - SwahiliBunge-
(a) litapitia, kuunganisha na kurekebisha sheria za ardhi zilizopo;
(b) litapitia sheria za matumizi ya ardhi ya kisekta kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa katika Kifungu cha 60 (1); na
(c) litatunga sheria-
(i) ili kuelezea kiwango cha chini na cha juu cha ekari za ardhi zinazoweza kumilikiwa na watu binafsi;
(ii) ili kusimamia namna ambavyo ardhi yoyote inaweza kubadilishwa kutoka kwenye kipengele kimoja kwenda kingine;
(iii) itasimamia utambuzi na ulinzi wa mali ya wanandoa na haswa nyumba ya wanandoa wakati wa ndoa na wakati wa kuvunjika ndoa;
(iv) italinda, kuhifadhi na kutoa idhini ya ufikiaji wa ardhi yote ya umma;
(v) itawezesha uhakiki wa ruzuku zote au matumizi ya ardhi ya umma i li kujua usahihi na uhalali wake;
(vi) itawalinda tegemezi wa marehemu wenye maslahi katika ardhi yoyote, ikiwa ni pamoja na masilahi ya wanandoa katika umiliki halisi wa ardhi;
… (Kifungu cha 68)
Property, Inheritance and Land Tenure
Kenya
- English...
(4) The provisions of this Chapter12 on equality shall be qualified to the extent strictly necessary for the application of Muslim law before the Kadhis’ courts, to persons who profess the Muslim religion, in matters relating to personal status, marriage, divorce and inheritance.
… (Art. 24) - Swahili...
(4) Vifungu katika Sura hii kwa usawa vitatumika kwa kiwango ambacho ni lazima kabisa kutumia sharia ya Kiislamu mbele ya mahakama za Kadhi, kwa watu ambao ni waumini wa dini ya Kiisilamu, katika maswala yanayohusu hadhi binafsi, ndoa, talaka na urithi.
… (Kifungu cha 24)
Property, Inheritance and Land Tenure
Kenya
- EnglishPrivate land consists of —
(a) registered land held by any person under any freehold tenure;
(b) land held by any person under leasehold tenure; and
(c) any other land declared private land under an Act of Parliament. (Art. 64) - SwahiliArdhi yenye umiliki binafsi inajumuisha -
(a) ardhi iliyosajiliwa ambayo inamilikiwa na mtu yeyote chini ya umiliki wowote chini ya muda usiokuwa na kikomo;
(b) ardhi inayomilikiwa na mtu yeyote chini ya umiliki wa kukodisha; na
(c) ardhi nyingine yoyote iliyotangazwa kuwa ni ya umiliki binafsi chini ya Sheria ya Bunge. (Kifungu cha 64)
Protection from Violence
Kenya
- English(1) A person shall not be held in slavery or servitude.
(2) A person shall not be required to perform forced labour. (Art. 30) - Swahili(1) Mtu hatashikiliwa katika utumwa au kutumikishwa.
(2) Mtu hatalazimishwa kufanya kazi ya shuruba. (Kifungu cha 30)
Protection from Violence
Kenya
- EnglishEvery person has the right to freedom and security of the person, which includes the right not to be—
…
(c) subjected to any form of violence from either public or private sources;
(d) subjected to torture in any manner, whether physical or psychological;
(e) subjected to corporal punishment; or
(f) treated or punished in a cruel, inhuman or degrading manner. (Art. 29) - SwahiliKila mtu ana haki ya uhuru na usalama wa mtu huyo, ambayo ni pamoja na haki ya-
…
(c) kutoingizwa kwenye aina yoyote ya vurugu kutoka ama vyanzo vya umma au vya binafsi;
(d) kutoingizwa kwenye mateso kwa njia yoyote ile, iwe ya kimwili au ya kisaikolojia;
(e) kutopewa adhabu ya viboko; au
(f) kutotendewa au kutoadhibiwa kwa njia ya kikatili, au ya kudhalilisha. (Kifungu cha 29)
Protection from Violence
Kenya
- EnglishDespite any other provision in this Constitution, the following rights and fundamental freedoms shall not be limited—
(a) freedom from torture and cruel, inhuman or degrading treatment or punishment;
(b) freedom from slavery or servitude;
… (Art. 25) - SwahiliLicha ya vifungu vingine vyovyote katika Katiba hii, haki zifuatazo na uhuru wa msingi hazitawekewa mipaka-
(a) uhuru dhidi ya kuteswa na ukatili, kitendo au adhabu ya udhalilishaji;
(b) uhuru dhidi ya utumwa na kutumikishwa;
… (Kifungu cha 25)
Protection from Violence
Kenya
- English...
(2) A political party shall not—
(a) be founded on a religious, linguistic, racial, ethnic, gender or regional basis or seek to engage in advocacy of hatred on any such basis;
(b) engage in or encourage violence by, or intimidation of, its members, supporters, opponents or any other person;
… (Art. 91) - Swahili...
(2) Chama cha siasa-
(a) hakitaanzishwa kwa msingi wa kidini, lugha, rangi, kabila, jinsia au kikanda au kujihusisha katika uenezi wa chuki kwa msingi wowote kama huo;
(b) kujihusisha au kuchochea vurugu kwa, au kutishia wanachama wake, wafuasi, wapinzani au mtu mwingine yeyote;
… (Kifungu cha 91)