Search Database

The Global Gender Equality Constitutional Database is a repository of gender equality related provisions in 194 constitutions from around the world. The Database was updated in partnership with the International Bar Association's Human Rights Institute (IBAHRI) and with support from the Swedish International Development Agency (SIDA) and the Government of Japan. Experience its wealth and depth of information by starting your search now.

REFINE RESULTS
About 143 results

Employment Rights and Protection

Kenya, Swahili

(1) Kila mtu ana haki ya kufanya kazi kwa usawa.
(2) Kila mfanyakazi ana haki -
(a) ya kupata mshahara mzuri;
(b) ya kuwa na mazingira mazuri ya kufanya kazi;
… (Kifungu cha 41)

Employment Rights and Protection

Kenya, Swahili


13. Viwango vya kazi.
… (Kiambatisho cha Nne - Mgawanyo wa Majukumu baina ya Serikaili ya Kitaifa na Serikili za Kaunti, Sehemu ya 1 - Serikali ya Kitaifa)

Sexual and Reproductive Rights

Kenya, Swahili

(1) Kila mtu ana haki ya kuishi.
(2) Maisha ya mtu huanza wakati wa kutungwa mimba.
(3) Mtu hataondolewa maisha kwa kukusudia, isipokuwa kwa kiwango kilichoidhinishwa na Katiba hii au sheria nyingineyo iliyoandikwa.
(4) Utoaji wa mimba haruhusiwi isipokuwa, kwa maoni ya mtaalamu wa afya, kuna haja ya matibabu ya dharura, au maisha au afya ya mama iko hatarini, au ikiwa inaruhusiwa na sheria nyingine yoyote iliyoandikwa. (Kifungu cha 26)

Sexual and Reproductive Rights

Kenya, Swahili

(1) Kila mtu ana haki -
(a) ya kuwa na afya ya kiwango cha juu zaidi, ambacho hujumuisha haki ya kupata huduma za afya, ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya uzazi;
… (Kifungu cha 43)

Minorities

Kenya, Swahili

(1) Tunu na kanuni za utumishi wa umma ni pamoja na—

(i) kupata fursa sawa na stahiki kwa ajili ya uteuzi, mafunzo na maendeleo, katika ngazi zote za utumishi wa umma, wa-

(ii) watu wa makundi yote ya makabila;
… (Kifungu cha 232)

Minorities

Kenya, Swahili


• “jamii ya pembezoni” humaanisha-
(a) jamii ambayo, kwa sababu ya idadi ndogo ya watu wake au kwa sababu nyingineyo yoyote, imeshindwa kushiriki kikamilifu katika maisha ya kijamii na kiuchumi ya Kenya kwa ujumla;
(b) jamii ya jadi ambayo, kutokana na hitaji au shauku ya kuhifadhi utamaduni na utambulisho wake wa kipekee na kitambulisho ili usipotee, imebaki nje ya maisha ya kawaida ya kijamii na kiuchumi ya Kenya kwa ujumla;
(c) jamii asilia ambayo imeshikilia na kudumisha mtindo wa maisha ya jadi na kujipatia riziki katika uchumi wa uwindaji na uokotaji; au
(d) watu na jamii ya wafugaji, iwe ni-
(i) wa kuhamahama; au
(ii) jamii yenye makazi ya kudumu ambayo, kwa sababu ya kujitenga kwake kijiografia, imeshiriki kidogo sana katika maisha ya pamoja ya kijamii na kiuchumi ya Kenya kwa ujumla;
"Kikundi cha pembezoni" humaanisha kikundi cha watu ambao, kwa sababu ya sheria au desturi za hapo awali, au baada ya tarehe ya utekelezaji walikuwa au wametengwa, kwa kubaguliwa kwa sababu moja au zaidi zilizopo katika Kifungu cha 27 (4);
… (Kifungu cha 260)

Minorities

Kenya, Swahili

Malengo ya ugatuzi wa serikali ni-

(d) kutambua haki ya jamii kusimamia mambo yao wenyewe na kukuza maendeleo yao;
(e) kulinda na kuimarisha masilahi na haki za watu wenye uwakilishi mdogo katika jamii na jamii za pembezoni;
… (Kifungu cha 174)

Minorities

Kenya, Swahili

Kanuni zifuatazo zitaongoza nyanja zote za fedha za umma katika Jamhuri
...
(b) mfumo wa fedha za umma utaimarisha jamii yenye usawa, na haswa-

(iii) matumizi yataimarisha maendeleo sawa ya nchi, ikiwa ni pamoja na kutunga sheria maalumu kwa ajili ya makundi na maeneo ya pembezoni;
… (Kifungu cha 201)

Minorities

Kenya, Swahili

...
(3) Vyombo vyote vya Serikali na watumishi wa umma wana wajibu wa kushughulikia mahitaji ya makundi yaliyopo katika mazingira hatarishi katika jamii, ikiwa ni pamoja na wanawake, wazee, watu wenye ulemavu, watoto, vijana, wanajamii wenye uwakilishi mdogo katika jamii au watu waliotengwa na jamii, na watu wa jamii ya kabila, dini au utamaduni fulani.
… (Kifungu cha 21)

Minorities

Kenya, Swahili


(3) Serikali ya kitaifa inaweza kutumia Mfuko wa Usawa-

(b) ama kwa dhahiri, au si kwa dhahiri kupitia ruzuku zenye masharti kwenda kwenye kaunti ambazo kuna jamii za pembezoni.
… (Kifungu cha 204)